Swahili
HABARI MPYA SIASA

Niwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2014 -Frank

Baada ya Chama cha demokrasi na kuhifadhi mazingira(DPGR) nchini Rwanda kupoteza kura kwa urahisi katika kinyang’anyiro cha kiti cha urais mwenyekiti wa cha hicho , Dkt. Frank Habineza, ametangaza kuwa ameshaamua kuwania tena muhula ujao ktk mwaka wa 2024.

Habineza ameweza tu kuchukua nafasi ya 3 na kura asilimia 0.48 katikauchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 4 mwezi huu. Ameshindwa na wagombea; Philippe Muhayimana(mgombea wa kujitegemea) na kura asilimia 0.73 na wa chama cha RPF-Inkotanyi Paul Kagame ameshinda kwa kipigo kikubwa cha kura asilimia 98.79.

Kwa mahojiano na gazeti la new times wiki hii, amesema kwamba ingawa chama chake hakikufanya vizuri katika uchaguzi huu, jambo hilo halitawafanya kukata tamaa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Ni wazi mno tunahuzunishwa na matokeo lakini ndivyo demokrasi inafanyika. Kuna mshinde na mshindi. Tunatarajiwa kujikusanya tena ili kuandaa uchaguzi ujao wa 2024. Tunaenda kuandaa kwa hudi na uvumba. Hatutahofia tena changamoto yoyote ile. Tunajua si rahisi ila hatutakata tamaa,” amesema

Ameongeza, Habineza, kuwa chama chake kiko tayari kwa uchaguzi wa bunge utakaofanyika mnamo mwezi wa nane mwaka kesho.

“Matokeo ya mwaka huu hayatatukatisha tamaa kwa ndoto zetu kuongoza nchi. Kuna mahali mengi ambapo katika kampeni zetu tulipohudhuria msongano wa watu. Tumeshangazwa na waliotuunga mkono, kwa mfano, Musanze na Kigali inaonyesha kuwa watu walikuwa wakivutiwa na sera zetu kwa hivyo tunapanga kurejea na kuwaomba waendelee kustahimili nasi,” amesema.

Habineza amesisitiza kuwa chama chake huenda watumia uzoefu waliounyakua kwenye kampeni kwa waungaji mkono nchini kote.

“Ni mara ya kwanza ya chama chetu kupatika kwa karatasi ya kura ya siri na tuliweza kufahamika mahali pote , watu wengi wameweza kujua kuhusu chama chetu na itikadi yetu nadhani tumetoa athari Fulani ya kidemokrasia na hatutasahaulika hivi punde,” ameongeza.

Habineza tena amempongeza rais Kagame kwa ushindi na anamwomba kutafakari sera za chama chake cha Green kwani lengo lilikuwa ni kujengea  kwa yale ambayo yameshafanyika.

Takribani watu miliyoni 6.8 ndio walioshiriki uchaguzi wa mwaka huu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com