kwamamaza 7

Nitauboresha uhusiano wa Rwanda na Burundi, Ufaransa na Kongo- Dkt Frank

0

Mgombea wa chama cha Green Dkt Frank Habineza ambaye anawania kiti cha Urais wa Rwanda katika uchaguzi utakaofanyika hapo mwezi ujao anaahidi kwamba ataweka kipaumbele kuuboresha uhusiano wa Rwanda mataifa mengine.

Dkt. Frank Habineza alisema haya akiwa katika mahojiano na vyombo vya habari baada ya kufanya kampeni zake katika wilaya ya Rubavu na Rutsiro na kusema atashughulikia hilo kwani alikutana na pingamizi hiyo pekee yake.

“tumetilia mkazo kwenye swala la uhusiano wa kidiplomasia na nchi ya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ili wakati ukifika tuweze kuweka mfumo wa kushirikiana kukilengwa kuwarahisisha watu kuendesha biashara zao kati yao bila pingamizi”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Dkt. Frank alisema kwamba yeye pekee alikutana na athari zinazohusiana na swala hili kwa kuwa miaka si mingi iliyopita alisafiri nchini Kongo na pasipoti yake ikashikiliwa na akaanza kuhojia akishukiwa kuwa jasusi.

Alisisitiza kwamba hiyi ndiyo sababu ataweka nguvu katika kuwarejesha wanyarwanda walioko uhamishoni na hata kutafuta jinsi ya kuondoa swala la uhusiano mbaya ulioko kati ya Rwanda na nchi za Burundi na Ufaransa.

Nchi kama Burundi imekuwa na uhusiano mbaya na Rwanda baada ya nchi hii kuushtaki utawala wa Rwanda kuhusika na machafuko yaliyotokea nchini humo baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza kwamba atawania muhula wa tatu. Nchi ya Kongo nayo imekuwa ikishtakiwa na Rwanda kuwaunga mkono wanamgambo wa FDLR ambao wanajificha kwenye misitu ya Kongo. Ufaransa nao haukuwa na uhusiano mzuri kwa kipindi cha miaka 23 iliyopita baada ya serikali inayotawaliwa na RPF Inkotanyi kuwashtumu wafaransa kuhusika na mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi ya mwaka 1994.

Uhusiano huo umekuwa na athari za moja kwa moja kwa raia wa nchi hizo mbili walikuwa na tabia ya kutembeana na majirani zao na hata kuendesha biashara kati yao.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.