Home HABARI Nitaendelea na shughuli za siasa – Mpayimana Philippe
HABARI - August 4, 2017

Nitaendelea na shughuli za siasa – Mpayimana Philippe

Baada ya kupiga kura, mgombea huru Mpayimana Philippe ameviambia vyombo vya habari kwamba kwamba amekwisha ufikia ushindi wake na linalobaki ni zamu ya wanyarwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mpayimana Philippe ambaye ndiye mgombea binafsi pekee katika uchaguzi huu ametangaza haya kwa wandishi wa habari alipokuwa anamaliza kupiga kura kwenye kituo cha Kura cha Camp Kigali mjini Kigali.

akipiga kura

Alipoulizwa imani yake ya kushinda uchaguzi amesema “ushindi nimekwisha jipatia nilichokuwa nasaka ni demokrasi na uhuru wa wanyarwanda kwa kuwa nimekwishayafikia haya yote, linalobaki ni kwa wanyarwanda yatakayotoka uchaguzi ni kwa ajili ya wanyarwanda”

Ingawa Philippe Mpayimana ana wasimamizi 100 tu nchini kote ana imani uchaguzi utakuwa wa haki na uwazi.

Alipoulizwa mpango wake wakati hatokuwa na bahati ya kushinda uchaguzi Mpayimana alijibu kwamba ataendelea na shughuli zake zaa siasa kwa kupambania haki na uhuru wa wanyarwanda na kuwa angegombea pengine mwaka wa 2024.

Swala la kwamba ataendesha shughuli zake za siasa nchini Rwanda aukwenye nchi za kigeni alilijibu kwingine Mpayimana kwa kufafanua kwamba ambalo wanapaswa kulijua kwanza ni kwamba wanyarwanda wote ni sawa wawe wanaishi ndani au nje ya nchi.

Mpayimana Philippe alirudi Rwanda Januari 2017 kuwania kiti cha urais baada ya miaka mingi alipokuwa akiishi nchini Ufaransa.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.