Swahili
SIASA

Ningependa uchunguzi kufanyika kwa wale wanaotatiza kampeni za wagombea urais- Waziri Kaboneka

Waziri wa utawala wa mitaa, Francis Kaboneka

Françis Kaboneka Waziri wa utawala wa ndani ya nchi ameomba viongozi wa ngazi za chini za nchi kuendelea kuwarahisisha wagombea kwa kampeni zao na hata kuagiza uchunguzi kufanyika kwa wale waliotatiza shughuli za wagombea.

Waziri Kaboneka ametangaza haya alipokuwa akiongea kwenye kipinda cha RBA ambapo amesema kuwa viongozi wa ngazi za chini walipewa masharti ya kuwaongoza nyakati hizi za kampeni na ambapo watashindwa watachukuliwa hatua.

Waziri huu alijibu kuhusu haya kufuatia madai yaliyozushwa siku za hivi karibuni na mgombea wa chama cha Green Dkt. Frank kuwa Kampeni zake zilitatizwa na viongozi wa ngazi za chini kama ilivyokuwa wilaya ya Nyagatare na kufanya kampeni zake kutofanyika hapo kufuatia kubadilishwa badilishwa kwa mahali palipokuwa pakitarajiwa kuendesha kampeni.

Kuhusu madai haya, mgombea Dkt. Frank aliomba hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya viongozi waliofanya shughuli zake kushindikana ikiwemo hata kuondolewa uadhifani.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa kujibu haya Waziri Kaboneka alisema

“Ningependa kuchukua fursa hii kuwaomba viongozi ambao wamekuwa wakijitia mwa makosa haya kusitisha na ngazi husika zinaombwa kuendesha uchunguzi na yeyote atakayepatikana na kosa kuchukuliwa hatua”

Waache wagombea na fursa yao ya kueleza mipango yao kwa wagombea ili wananchi waje wakafanye maamzi yao kuhusu nani kumpa kura, kulingana na mipango yao.

Waziri vilevile alipata fursa ya kuwahimiza viongozi wanaositisha shughuli zao za kila siku kwa ajili ya kampeni za mgombea yeyote kuacha.

“Ikiwa kuna pale jambo hili linapotokea na ikiwa kuna wale wanaotaka kwenda kampeni wasiende wote kwa kuwa kuna watu kutoka maeneo ya mbali wanaokuja kutafuta huduma zao. Fikiria kuhusu mtu anayetoka safari ya mbali akija kutafuta huduma na akakosa”

Aliwahimiza pia waendesha shughuli za kibinafsi kwamba haifai kusitisha kazi kwa ajili ya shughuli za kampeni. Hapa alisema kuwa waendesha biashara ya migahawa, na maduka wangepata fursa hii kuuza bidhaa zao kwa wingi kwa kuwa huwa na wateja wengi wanaokuja kuhudhuria kampeni.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wagombea ambao wanawania kiti cha urais ni Paul Kagame ambaye anawania kwa tiketi ya chama cha RPF, Dkt. Frank Habineza ambaye ni mgombea wa chama cha Green na hata Phillipe Mpayimana , mgombea binafsi pekee.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com