Swahili
DINI

Ni nini Baba Muumbaji anataka ushike moyoni mwako?

Dunia inaomboleza,inazimia,ulimwengu unadhoofika,unazimia,watu wakuu wa dunia wanadhoofika.tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa,kwa maana wameziasi sheria,wameibadili amri.wamelivunja agano la milele.Ndiyo sababu laana imeila dunia hii,na watu wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia,ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea,watu waliosalia wakawa wachache tu” ISAYA 24:4-6

Mpendwa msomaji,tafakari sana aya hizi za utangulizi.

Unaweza kuungana na kile maandiko yanachoonyesha kuhusu hali halisi ya Dunia yetu hii leo.

Laana inaila dunia yetu hii leo kwa sababu zifuatazo

 1. “Wameziasi sheria”
 2. “Wameibadili amri”
 3. “wamelivunja agano la milele”

Hivyo katika waraka huu, mungu anahitaji kutuonyesha namna ya kuepukana na laana hiyo.ila tu nai mpaka pale tutakapogundua mambo yafuatayo:-

 1. Amri hizo za mungu ni zipi?na ni ngapi?
 2. Amri hizo za mungu ni za muhimu mpaka sasa?(kizazi hiki)
 3. Amri hizo za mungu,kila mtu anapaswa kuzijua na kuzitii? Na anwajibishwa kwa kutozifahamu au kuzivunja? Kwa hayo na yanayotokana na hayo ndiyo lengo la waraka huu.mungu akubariki uanaposoma Neno Lake.

AMRI ZA MUNGU NI ZIPI NANI NGAPI?

 1. Usiwe na miungu mingine ila mimi.KUTOKA 20:3
 1. Usijifanyie sanamu ya kuchonga,wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni,wala kilicho chini duniani,wala kilich majini chini ya dunia.usivisujudie wala kuvitumikia;kwa kuwa  mimi ,BWANA Mungu wako ni Mungu mwenye wivu;nawapatiliza wana maovu ya baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne chawanichukiao,name nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu.KUTOKA 20:4-6
 1. Usilitaje bure jina la BWANA,Mungu wako maana BWANA hata mhesabia kuwa hana hatia mtu alitajae jina lake bure.KUTOKA 20:7
 1. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.Kwa siku sita utafanya kazi zako zote, lakini siku ya saba ni Sabato kwa BWANA Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yo yote, wewe wala mwana wako au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.Kwa kuwa kwa siku sita, BWANA aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.KUTUKA 20:8-11.Katika  amri ya nne,tunaagizwa kuitunza sabato.

SABATO NI SIKU IPI?

Biblia inatuambia kuwa sabato ni siku ya saba katika wiki.biblia inasema :-

“Baada ya siku ya sabato, maria Magdalena, salome na maria mama yake yakobo walinunua manukato ili waupake mwili wa yesu .basi alfajiri na mapema siku ya jumapili,walifika kaburini,jua lilipoanza kuchomoza”.

MARKO 16:1-2(BIBLIA-HABARI NJEMA, KISWAHILI CHA KISASA)

Hivyo hapo na habari ya ufufuko wa Yesu,tunaona kuwa alifufuka jumapili amboyo ndiyo siku ya kwanza  ya juma soma MATHAYO 28:1

Ø  Pia biblia inatuonyesha siku ya kifo chake,ilikuwa ijumaa ambayo ndiyo maandalio ya sabato.

“Siku hiyo ilikuwa ijumaa,na maandalio ya siku ya sabato yalikuwa yanaanza .wale wanawake walioandamana na yesu kutoka  Galilaya walimfuata Yosefu, wakaliona lile kaburi na jinsi mwili wake Yesu ulivyowekwa .Halafu wakarudi nyumbani,wakayatayarisha manukato na marashi ya kuupaka mwili wa Yesu .Siku ya sabato walipumzika kama ilivyoamriwa na sheria”LUKA 23:54-56

Kwahiyo tunaona kuwa sabato siyo ijumaa wala Jumapili bali ni Jumamosi

 1. Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa   BWANA Mungu wako.KUTOKA 20:12
 1. Usiue. KUTOKA 20:13
 1. Usizini. KUTOKA 20:14
 1. Usiibe. KUTOKA 20:15
 1. Usitoe ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yako. KUTOKA 20:16
 1. Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ng’ombe wake au punda wake wala cho chote kile alicho nacho jirani yako. KUTOKA 20:3-17, KUMBUKUMBU LA TORATI 5:7-21

Ø  Amri za Mungu ni za muhimu kwa Nyakati zote na vizazi vyote.Yesu anatoa agizo hili juu ya umuhimu wa amri za Mungu:-“……………………….lakini ukitaka kuingia katika uzima zishike amri MATHAYO 19:17

“Msidhani kwamba nimekuja kuondoa Torati au Manabii, sikuja kuondoa bali kutimiza.Kwa maana,amin, nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe kimetimia. Kwa hiyo, ye yote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme ya Mbinguni.Kwa maana nawaambia, haki yenu isipozidi haki ya waandishi wa sheria na Mafarisayo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni”.MATHAYO 5:17-19

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Ø  Watu wengi leo ,hutoa udhuru wa kuzishika Amri kumi za Mungu,kwa madai ya kumwamini na kumpenda Yesu.Husema “Ukimwamini Yesu tu,inatosha,hakuna haja ya kuzishika amri”.je, udhuru huo Yesu aliukubali katika maandiko matakatifu?

Yesu mwenyewe alisema;-

Mkizishika amri Zangu mtakaa katika pendo Langu, kama Mimi nilivyozishika amri za Baba Yangu na kukaa katika pendo Lake.”YOHANA 15:10

“Kama mnanipenda, mtazishika amri Zangu.”YOHANA 14:15

Kwa kuwa huu ndio upendo wa Mungu, kwamba tuzitii amri Zake. Nazo amri Zake si nzito”.1YOHANA 5:3

Ø  Je amri za Mungu kila mtu anapaswa kuzijua na kuzishika? Au kwa ajili ya watu Fulani tu,au dhehebu Fulani tu?

Biblia Inasema:-

“Hii ndiyo ya maneno ;yote yamekwesha sikiwa,mche mche Mungu, nawe uzishike amri zake maana kwa jumla ndiyo impasavyo mtu “MHUBIRI 12:13

Hivyo tunaona kuwa biblia inasema kuzishika amri za mungu kunampasa kila mtu yeyote anayejifahamu kuwa yeye ni mtu ‘ anapaswa kuzishika amri za mungu. Hata kama mtu angesema’Mima nampenda mungu’ au mimi nimeokoka; kama bado hataki kuzishika Amri za mungu ;madai yake huyo hayaungwi mkono na Biblia kwan maandiko yanasema”

Wokovu u mbali na wasio haki’ kwa maana hawajifunzi amri zako ZABURI 119:115

‘’Umewakataa wote wazikosao amri zako ,kwa maana hila zao ni uongo’’ZABURI 119:118

‘’Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye ikiwa tunashika amri zake.Yeye asemaye nimemjua ,wala hazishiki amri zake,ni uongo wala wala kweli haimo ndani yake’’YOHANA2:34.MITHALI28:9

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com