kwamamaza 7

Ngoma: Wizi ni matokeo ya ukosefu wa chakula

0

Wanaoishi tarafa ya Zaza, Mugesera pamoja na Sake katika wilaya ya Ngoma, wanasema kwamba kumetokea aina ya wizi pakiwemo kubomoa manyumba, uongozi huona kuwa ni matokeo ya mavuno yaliyo kuwa machache mwaka jana na msaada walio kubaliya wakaaji imekoma.

Katika viini ya tarafa hizo hakuna hata siku moja inayoweza kucha bila kusikia kwamba mahali fulani wamebomoa nyuma, wameiba fugo au kusikia kwamba wamekama mtu akivuna mavuno yasiyokuwa yake.

Sehemu ijulikanayo kwa jina la Kibare, kiini Nyamugari, tarafa Mugesera, huko wizi huchinjia fugo mahali walilo liiba na wanatwala machinjo, ingine ya kushangaza ni kwamba wanafikia hatua ya kuiba hata vifaa vya jikoni.

Kiongozi wa kijiji cha Gishandaro, Maniragena Esperance eti “siku chache walibomoa nyumba ya Bigirabake Efreim, wakaingia jikoni na kutwaa hata safuriya za jikoni na viatu”.

Katika tarafa hizo za Gisaka, kuna wizi wanao ingia nyumbani wanatisha wenyeji wakiwaomba wanavyo hitaji ili wasiwaharibie maisha.

Raia wanasema kuwa wizi hauwezi kukoma kwa sababu hawaazibiwi, wakati wanaiba, wakikamatwa na kupigwa mwenye mali ndiye anaazibiwa, mafano wanasema kuna aliye kamatwa akiiba mihogo katika kijiji ya Rwabutare, mwenyeji akamutupia jiwe, eti “ mwizi yupo kwenye matibabu na mwenyeji akiwa gerezani huko Zaza”.

Kiongozi anayehusika na ukulima katika tarafa ya Mugesera, Ngirumuhire Jean Baptiste, anahakikisha kwamba wizi umezuka tena. Sababu ya wizi huo ni ukosefu wa chakula wa siku nyingi katika wilaya na umasikini, msaada ambao wakaaji walikuwa wakipewa siku nyingi hawapati tena.

Kiongozi huo huendelea na kusema kwamba hata maharagi waliolima mashambini wamepatwa na ukosefu wa mvua, hata kuna wadudu wanao haribu mavuno ya mahindi.

Juma tatu tarehe 17 April, kiongozi wa wilaya ya Ngoma, Nambaje Aphrodise alitembelea tarafa ya Mugesera, baada ya watu wasio julikana kukata ng’ombe ya Cyanzayire Agnes siku ya juma pili. Hakusema ujumbe aliotoa kwenye simu yake ya mkononi, aliye shika simu ni mwenye kuhusika na maisha bora ya raia ila hakujua mambo ya ziara ya kiongozi wake.

Katika wilaya hio watu wanao omba omba njiani wameongezeka, wakisema lugha ya Kirundi ili wakaaji wafikiliye kuwa ni wakimbizi na ikiwa majirani yao.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Leki

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.