kwamamaza 7

Ngoma: Watu 4 walikamatwa wakitumia katani na wakiwa na kilo 165

0

Tarehe 29 Januari 2017, polisi ya Rwanda katiaka wilaya ya Ngoma iliwakamata watu wane wakivuta katani na mmoja wao alikua na mifuko nne ya katani yote ikiwa na kilo 165.

Waliokamatwa ni Havugabaramye Jonas, Ibyimanikora Jean Baptiste, Niyonsaba Jean Baptiste pamoja na Uwiringiyimana.

Msemaji wa polisi jimbo la Mashariki, Inspector of Police (IP) Emmanuel Kayigi amesema kuwa waliwakuta wakivuta katani katika nyumba ya Ibyimanikora mwenyeji wa kiini ya Kinyonzo, tarafa ya Kazo. Walikwenda kusaka katika nyumba ya Havugabaramye ndipo wakaona hio katani kilo 165 na ndipo mhusika akasema kuwa alimuwekea Ibyimanikora.

[xyz-ihs snippet=”google”]

IP Kayigi eti,”kukamatwa kwa hao ni kutokana na taarifa kutoka kwa wakaaji, ikimaanisha ya kua raia tayari wamejua matokea mabaya ya katani, nawashukuru kwa hayo”, na akiwaomba kuendelea kutoa taarifa ili kuzuia usambazaji wa dawa za kulevya.

Hao wane wapo kwenye stesheni ya polisi ya Mutenderi hata hio katani kilo 165 huwekea hapo na upelelezi ukiendelea.

Msemaji wa polisi jimbo la mashariki amewapa ujumbe akisema kuwa wanajuwa mbinu ambazo hutumia ili kufanya biashara ya dawa za kulevwa, na kuambia wakaaji kuwa wakisubutu watakamatwa bila shaka.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.