kwamamaza 7

Ngoma: Raia waumizwa na viboko wanakula mazao

0

Raia wa wilaya ya Ngoma katika mkoa wa mashariki mwa Rwanda hulalamika kwa ajili ya viboko ambao hutoka wanakula mazao. Wanaokabiliwa zaidi ni raia wanaoishi katani Jarama ambao huwakuta viboko katika mimea na kuna wakati hukutania nyumbani.

Viboko hutoka mtoni Akagera na kula mimea na mazao ya raia mithili ya mahindi, maharagwe, nk hivi hawategemei kupata mavuno.

Mmoja mwa raia, Turikumwenimana Leopold alisema kwamba viboko wamekula shamba nzima la mahindi. “Hapa viboko hula mimea na mazao, walikula mahindi shambani ambapo niliweka pesa za Rwanda 40,000; sitapata mavuno kabisa.”

[ad id=”72″]

Wasiwasi za wananchi kukosa uongozi na shirika zenye kuwajibika na madai ya fidia. Mmoja alisema, “Ni wapi unaweza kuelekea wakati kiboko amekula mazao na mimea yako? Ni wapi unaweza kuwashtaki wanyama?” Aliongeza kwamba wanajikusanya ili kuomba malipo serikali.

Mulisa Japhet, Kiongozi wa kata ya Jarama ambayo hukabiliwa zaidi alisema kwamba hakuna raia aliyeleta madai ya fidia kuhusu wanyama hawa ijapokuwa alisikia fununu za wanyama kula mazao ya raia. Aliongeza kwamba uongozi wa kata utawafanyia utetezi katika bodi ya maendeleo.

Bodi ya maendeleo ya Rwanda (RDB) huwapatia fidia waathirika ambao mazao yao yamehalibiwa na wanyama wa mbuga baada ya kuhesabu thamani ya hasara.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.