kwamamaza 7

Nduguye Rais Museveni adaiwa kumsaidia kutoroka Jen. Kayumba Nyamwasa

0

Nduguye Rais Museveni, Jen. Caleb Akandwanaho maarufu Salim Saleh amedaiwa kumsaidia Jen. Kayumba Faustin Nyamwasa aliyetoroka nchini Rwanda tarehe 25 Julai 2010.

Kwa mujibu wa taarifa za Great Lakes Watchman Jen. Kayumba alikuwa akishirikiana na Jen. Salim Saleh kabla ya kutoroka.

Hizi taarifa zinasisitiza Kayumba alivuka  mpaka wa Rwanda na Uganda kinyume na sheria na kukaribishwa na Salim Saleh Wilayani Masaka, nchini Uganda.

Huyu alibebwa na magari ya aina ya Landcruiser na kumpeleka mjini Kampala.

Moja mwa haya magari alikuwemo jen. Salim Saleh. Huyu alisaidiwa kufika kwenye mpaka wa Uganda na Kenya huko Busia kisha akaondoka nchini Afrika Kusini.

Pia Jen. Salim Saleh anatuhumiwa kumuanga mkono kibiashara tajiri Tribert Ayabatwa Rujugiro ambaye inasemekana kwamba ni mdhamini wa chama cha Jen. Kayumba, Rwanda National Congress (RNC).

Kwa upande mwingine, tutatafuta mbinu za kuhojiana na  Jen. Salim Saleh ili kuzungumzia kuhusu haya madai.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.