kwamamaza 7

Nduguye Jenerali Kayumba Nyamwasa aitaka mahakama kuhukumu kesi yake hadharani

0

Nduguye Jenerali Kayumba Faustin Nyamwasa, Luteni Kanuni Rugigana leo 30 Aprili 2018 ameitaka mahakama ya juu nchini Rwanda kuhukumu kesi yake hadharani ili kutoa funzo kwa umma.

Lt.Kanuni Rugigana amesema haya baada ya mwendeshamashtaka Cpt.Faustin Nzakamwita kutoa ombi la kuwa kesi hii haistahili kutokea hadharani kwa kuwa ina uhusiano na usalama wa nchi.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Mshitakiwa ameeleza haelewi kwa nini kesi yake haiwezi kutokea hadharani wakati ambapo kuna kesi sawa na yake ambazo zilitokea hadharani. Rugigana amesema kuwa kama anayoshtakiwa ni ukweli,wangelikubali kesi yake kuhukumiwa hadharani.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Pia amesisitiza anayoshtakiwa ni uongo mtupu na kuwa ombi la la mwendeshamashtaka  linahusudia kuficha makosa aliyoyafanya.

Mwanasheria wa Rugigana,Me Geoffrey Butera ameelezea jaji kwamba mwendeshamashtaka hakutoa sababu maalumu za kutohukumia kesi hii hadharani.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Hatimaye,Mahakama imeamua kutohukumu kesi hii hadharani kutokana na uzito wa anayoshtakiwa Luteni Kanuni Rugigana.

Luteni Kanuni Rugigana alikamatwa mwaka 2011 na kuhukumiwa kufungwa jela miaka tisa na faini ya frw 100,000 lakini akapiga rufaa.Huyu alishtakiwa usaliti kwa nchi kupitia vita na kusambaza fununu zinazolenga kuzusha ghasia nchini.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.