kwamamaza 7

Ndizo hizi siri 7 za maombi yanayojibiwa

0

Musa alipoomba, Bahari ya Shamu iligawanyika. Eliya alipoomba, moto ulishuka kutoka mbinguni. Danieli alipoomba, malaika aliyafumba makanwa ya simba wale wenye njaa kali. Biblia inatueleza visa vingi vya kusisimua vya maombi yaliyojibiwa. Tena inapendekeza kwetu maombi kama njia ya kupata ule uweza kwetu maombi kama njia ya kupata ule uweza mkuu wa Mungu. Yesu anaahidi hivi: “Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nami nitalifanya” – (Yohana 14:14).

Lakini maombi mengine bado yanaonekana kana kwamba hayasikilizwi. Kwa nini? Hapa chini zipo kanuni saba zitakazokusaidia wewe kuomba kwa ufanisi zaidi:

  1. Uwe karibu sana na Kristo.
    “NINYI MKIKAA NDANI YANGU, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtapewa.” – Yohana 15:7.

Tunapoupa kipaumbele uhusiano wetu na Mungu na kuwa karibu naye, tutakuwa tunasikiliza na kutazamia kupata majibu kwa maombi yetu ambayo, vinginevyo, tusingeyatambua.

2.Endelea Kumtumaini Mungu.
“MKIAMINI, mtapokea yote myaombayo katika sala zenu” – (Mathayo 21:22).

Kuamini au kuwa na imani, maana yake ni kwamba tunamtazamia Baba yetu aliye mbinguni kwamba kweli atatupa hayo mahitaji yetu. Kama wewe una wasiwasi kwamba huna imani, basi, kumbuka kwamba Mwokozi alitenda mwujiza kwa mtu yule aliyemsihi sana akiwa amekata tamaa, aliyesema:”
“Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu!” – (Marko 9:24).

Wewe kazana tu kuitumia imani ULIYO nayo; usiwe na waiswasi juu ya imani ile usiyo nayo.

3.Jisalimishe kimya kimya chini ya mapenzi ya Mungu.
“Huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu cho chote SAWA SAWA NA MAPENZI YAKE, anatusikia” – (1 Yohana 5:14).

Kumbuka kwamba Mungu anataka kutufundisha sisi, pamoja na kutupa sisi vitu, kwa njia ya maombi. Kwa hiyo, wakati mwingine anatuelekeza upande mwingine. Maombi ni njia ya kutusogeza sisi zaidi na zaidi karibu na mapenzi ya Mungu. Hisia zetu zinatakiwa ziwe kali kutambua majibu ya Mungu na kujifunza kitu kutokana nayo. Kuyafuatilia kwa karibu maombi yetu fulani fulani ya pekee pamoja na kile kinachotokea kuhusiana nayo ni msaada mkubwa kwetu.

Roho Mtakatifu atakusaidia kulenga shabaha yenyewe: “Roho anawaombea watakatifu kulingana na mapenzi ya Mungu” (Warumi 8:27. Kumbuka kwamba mapenzi yetu yangeweza kulandana siku zote na mapenzi ya Mungu endapo sisi tungeweza kuona kama yeye anavyoona.

4.Mngojee Mungu kwa Saburi.
“NALIMNGOJA BWANA KWA SABURI, akaniinamia akakisikia kilio changu” – (Zaburi 40:1).

Jambo kubwa hapo ni kukaza mawazo yako yote kwa Mungu, kukaza mawazo yako yote juu ya suluhisho lake. Wala usithubutu kumwomba Mungu akusaidie kwa dakika moja, na halafu kujaribu kuzizamisha shida zako kwa kujifurahisha katika anasa dakika inayofuata. Umngoje Bwana kwa saburi; tunahitaji kuwa na nidhamu hiyo vibaya sana.

5.Usiinganganie Dhambi iwayo yote.
(“Kama ningalinuia maovu moyoni, Mwenyezi-Mungu hangalinisikiliza”)- Zaburi 66:18.

Dhambi ijulikanayo hukata mara moja uweza wa Mungu katika maisha yetu; inatutenga mbali na Mungu (Isaya 59:1-2). Huwezi kuishika na kuing’ang’ania dhambi kwa mkono mmoja na kunyosha mkono mwingine kupokea msaada wa Mungu. Ungamo la dhambi litokalo moyoni hasa pamoja na toba ya kweli ndilo suluhisho la tatizo hilo.

Kama sisi hatutaki kumruhusu Mungu kutuweka huru mbali na mawazo, maneno na matendo yetu mabaya, basi, maombi yetu hayawezi kutuletea jibu lo lote.

“Hata mwaomba, wala hampati, kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu” – (Yakobo 4:3).

Mungu hatajibu “ndiyo” kwa maombi ya uchoyo. Acha wazi masikio yako yapate kuisikia sheria ya Mungu [Amri Kumi], yaani, mapenzi yake, naye ataacha masikio yake wazi kuzisikia dua zako.

“Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria [Amri Kumi], hata sala yake ni chukizo” – (Mithali 28:9).

6.Tambua Kwamba Unamhitaji Mungu.
Mungu huwajibu wale wanaoomba kuwako kwake na uweza wake katika maisha yao.

“Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa.” – Mathayo 5:6.

7.Kuendelea Kuomba Tu.
Yesu alitoa kielelezo cha kuwapo kwa haja ya kuendelea tu kutoa dua zetu kwa kusimulia kisa kile cha mjane aliyekuwa anaendelea tu kuomba na kuendelea kuja kwa hakimu akiwa na ombi lake lile, lile. Mwishowe yule hakimu alisema, huku akiwa ameudhika vibaya sana, “Kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitahakikisha kwamba nampatia haki yake.” Kisha Yesu alitoa hitimisho lake hili: “Je! Mungu hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku? Je! atazidi kuahirisha kuwapatia haki yao?” (Luka 18:5-7).

Zungumza na Mungu juu ya mahitaji yako yote, matumaini yako yote, na ndoto zako zote. Omba mibaraka ya pekee, omba msaada unapokuwa na shida. Endelea kutafuta, tena endelea tu kusikiliza, mpaka ujifunze kitu fulani kutokana na jibu lake Mungu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.