kwamamaza 7

Ndege iliyobeba wachezaji wa timu ya soka ya Brazil yafanya ajali, Abiria 76 wafariki

0

Ndege iliyokuwa imewabeba watu 81, wakiwemo wachezaji na maafisa wa moja ya klabu kubwa za soka nchini Brazil, imeanguka ikikaribia mji wa Medellin nchini Colombia na kuua watu 76.

Ndege hiyo ilianguka eneo la milimani nje kidogo mwa mji wa Medellin majira ya saa sita usiku saa za huko (saa mbili asubuhi Afrika Mashariki) na Polisi wamesema watu watano walinusurika lakini watu wengine wote waliangamia.

[ad id=”72″]

Ndege hiyo ya kukodishwa ilikuwa safarini kutoka Brazil ikipitia Bolivia na ilikuwa imewabeba wachezaji na maafisa wa timu ya Chapecoense. Klabu hiyo ilikuwa imepangiwa kucheza mechi ya fainali ya Copa Sudamericana, dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya mji wa Medellin.

Wachezaji wa timu ya Chapecoense, Wawili tu wamenusurika
Wachezaji wa timu ya Chapecoense, Wawili tu wamenusurika

Mechi ya awamu ya kwanza ya kombe hilo, la pili kwa umuhimu Amerika Kusini, ilikuwa imepangiwa kuchezwa Jumatano lakini sasa imesitishwa.

Timu hiyo inayotoka mji wa Chapeco, kusini mwa Brazil, ilipandishwa kucheza ligi ya daraja ya kwanza nchini Brazil mwaka 2014 na ilifika fainali ya kombe hilo la Sudamericana kwa kulaza San Lorenzo ya Argentina.

[ad id=”72″]

Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (Conmebol) limesema kwamba limesitisha shughuli zake zote kwa sasa.

_92706662_8f73ddc2-137f-4da9-a8d4-068c9701ad7d

Taarifa zinasema ndege hiyo muundo wa British Aerospace 146 ambayo imekuwa ikitumiwa na shirika la ndege la Lamia la Bolivia ilikuwa na abiria 72 na wahudumu tisa.

Inasemekana kuwa watu wawili kutoka kwa timu hiyo – Alan Ruschel na Danilo – huenda wamenusurika.

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Jose Maria Cordova de Rionegro uliopo Medellin, wamesema juhudi zote zinafanywa kuwaokoa manusura na hali mbaya ya hewa inazuia maafisa kufikia eneo la mkasa kwa urahisi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter 

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.