kwamamaza 7

Mwizi apata pigo kupitia uchawi unaofahamika kama “uruhereko”

0

Mvulana anayeitwa Nshimiyimana Claude amejikuta matatizo alipoamka akiwa nyumbani kwa mwanamke aliyeibwa kwa kunyanganywa mkoba uliokuwemo vitu vingine vya thamani.

Imekuwa wiki mbili tangu mwanamke huyu anyanganywe mkoba wake uliokuwemo vitu vingine kama vitambulisho, simu za mkononi na hata fedha. Baada ya kuibiwa na mwizi akatoweka mwanamke huyu alipewa ushauri wa kumuendea mchawi wa “uruhereko” na kijana huyo akajikuta amerudi kuomba msamaha.

“Mara nikimwona nilimkaribia na kumnyanganya mkoba, sikumfahamu mke huyo awali ila nilihisi yeye anatoka Kigali hivyo nikakimbilia nilipofika mahali ambapo palikuwa salama nilitoa simu, na fedha na vitu vingine nikatupa mahali ambapo nilidhani wanatupa michafu” Mwizi asema.

Kayitesi Chantal mwenye kuibiwa yeye alisema alikwenda kwa mchawi kwa madhumuni ya kumgundua aliyeiba mkoba wake ila alikwenda hapo bila matumaini kwamba atampata, “Mtu mmoja alinisikia nikiwa nikinungunika na kuniambia usijali najua mtu ambaye atakusaidia, alinimwonyesha kwa hivyo mimi na mume yule tukawa na mazungumzo Fulani na akaniambia atanifanyia yangu”

Asubuhi ya siku ambayo mwizi huyo alipokwenda kwa Kayitesi ,walimwita wakimwuliza ikiwa amekwisha mwona mtu ambaye aliiba mkoba wake na alipomtupa macho tu mwizi akaanza  kuomba msamaha kwa ajili ya fedha alizoniiba kama Kayitesi anavyoeleza.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mwizi ninemwona ni mtu maskini asiyejiweza “ kulingana na vile mtu yule anavyoonekana hawezi kurudisha fedha zozote; sioni popote ambapo angeweza kupata fedha zile na ingekuwa bora akiniambia pale alipotupa mkoba wangu”

Mchawi mwenye jina la Rurangirwa Wilson kwa jina la umaarufu la Sarongo anasema ana dawa ambayo alitumia kumvuta mwizi yule amesema aliomba Polisi kumtia nguvuni mwizi yule lakini hali yake haikuwa nzuri kwa mjibu wa askari Polisi.

Mume huyu alikiri kwamba ana dawa hii yenye uwezo wa kumvuta mtu ambaye anathubutu kuiba na kumfanya kurudisha mali anayoiba. Aliendelea kusema kwamba ana pia uwezo wa kuwaambatisha pamoja mke na mume wanaofanya ngono ya nje ya ndoa lakini amesema pia hatowi dawa hii kiholela kwa sababu wangepata maafa ya ziada wanandoa husika.

Wananchi walipongeza aina ya uchawi huu kwa sababu haumuuwi yeyote bali unasaidia kupambana na wezi.

Mambo ya uchawi “uruhereko” kama huu yamekuwa akijitokeza kwa siku za hivi karibuni kwa kuwa kumeripotiwa kesi kadhaa mfano wa wilaya ya Bugesera ambako kesi mbili zilijitokeza na hata mtu aiyenata kwenye ndizi akitaka kupora.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter 

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.