Swahili
Home » Mwezi 1 mjini Kigali kulionekana makosa 500
HABARI

Mwezi 1 mjini Kigali kulionekana makosa 500

Makamu mwendesha mashtaka wa polisi ya Rwanda CSP Morris Murigo, amesema kuwa kwa mwezi huu wa Januari 2017, mjini Kigali kulionekana makosa zaidi ya 500 na tayari yamefikishwa mahakamani.

Mengi kati makosa hayo ni wizi, utumiaji wa dawa za kulevya, na vitambulisho kughushi.

Hayo yalitangazwa wakati wa kujadiliana kimafikiri kati ngazi tofauti tangu kijiji hadi wilaya katika wilaya ya Nayarugenge, ngazi za usalama na wizara ya utawala wa nchi (MINALOC).

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wilaya ya Gasabo ilichukuwa nafasi ya kwanza kwani ilikuwa na makosa 217, Nyarugenge nafasi ya pili na makosa 181, wilaya ya Kicukiro ikachukuwa nafasi ya tatu na makosa 108.

Kwa uwingi wa makosa hayo: wizi ni 105, kupiga na kujeruhi ni 99, dawa za kulevya 75, uwizi kimayele 36 na kubaka watoto ni 30.

Rwego Yussuf, kiongozi wa kijiji kati tarafa ya Nyarugenge amesema kuwa chanzo ya hayo yote ni utumiaji wa dawa za kulevya kwa kuwa mara nyingi wanao kamatwa walifikiwa na walitumia dawa za kulevya.

Makamu kiongozi mkuu wa polisi Rwanda DIGP Dan Munyuza aliomba wakaaji kuwa na mila kama usalama na hapo watazuia makosa, wakizuia ubiashara wa dawa za kulevya na kuwa na uwasiliano mwema na polisi.

Kosa lilingine amabalo hukama hatua na utumiaji wa vitambulisho kughushi ao haramu kwani mwezi huu wa Januari ilionekana makosa 18 na yote ikiwa na usamini wa miliyoni zaidi ya 700.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com