kwamamaza 7

Mwenedata naye ameamua kugombea urais Rwanda

0

Orodha ya wagombea urais watarajiwa nchini Rwanda inazidi kuwa ndefu, ambapo Gilbert Mwenedata aliyewania ubunge mwaka 2013 na kuanguka, naye ametangaza nia.

Alipata asilimia 0,4 katika uchaguzi wa wabunge ambapo alisimama kama mgombea binafsi.

Kuanguka kwake kwenye uchaguzi huo hakukumkatisha tamaa na sasa yuko tayari kuanza mbio za kusaka kiti cha urais.

“Wapiga kura ni Warwanda na kupata kura inategemea na sera zako, nina sera nzuri ambazo nina imani watazipenda,” amesema Mwenedata katika mahojiano na Habari Pevu.

Alipoulizwa misingi ya matumaini ya kupata dhamana ya kuiongoza Rwanda kupitia uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 4, 2017, Bw Mwenedata amejizuia kulijibu swali hilo.

Amesema yupo kwenye michakato ya kutafuta sehemu atakayofanya kikao na waandishi wa habari ambapo kwenye kikao chake ndipo atatangaza sera zake kwa mapana na marefu.

Akishapata kibali cha kufanya kikao na wanahabari ndipo atawasilisha nia yake kwa Tume Huru ya Uchaguzi, kwa mujibu wa maelezo yake.

Bwana Mwenedata ambaye ana umri wa miaka 42, amekuwa akifanya kazi na shirika la misaada la Marekani la USAID.

Rais Paul Kagame kutoka chama tawala cha RPF-Inkotanyi, Frank Habineza wa DGPR, Diane Rwigara na Philippe Mpayimana, nao wanatarajiwa kugombea urais.

Mwaka 2015 Katiba ya Jamhuri ya Rwanda ya mwaka 2003 ilirekebishwa ili kumwezesha Rais Kagame kuwania awamu ya tatu, ambapo anaweza kuongoza Rwanda hadi mwaka 2024.

Marekebisho hayo yalifanyika kupitia kura ya maoni kwa mapendekezo ya wananchi, ambapo raia walidai eti hakuna mtu mwingine awezaye kuiongoza Rwanda vizuri kama Rais Kagame.

Rais Kagame amekuwa Rais wa Rwanda tangu mwaka 2000 baada ya Pasteur Bizimungu kujiuzulu. Alichaguliwa miaka mitatu baadaye na mwaka 2010 pia.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.