Uongozi wa dini ya katoliki nchini Rwanda umemkemea padri Nahimana Thomas ambaye anasubiriwa kufika kwa nchi ya kizazi kesho katika jitihada za kushindania uongozi wa nchi katika uchaguzi utakaofanyika mwaka ujao, 2017.

Nahimana aliyekuwa padri katika dayosisi ya Cyangugu tangu 1999, alikuwa uhamishoni nchini Ufaransa baada ya kuhamia miaka kadhaa na kujiingiza katika mambo ya siasa akiwa kiongozi wa chama cha siasa ‘Ishema’.

[ad id=”72″]

Askofu wa baraza la maaskofu la kikatoliki nchini Rwanda, Philippe Rukamba, katika maomgezi na gazeti la KT Press alisema, “Tumemfukuza katika dayosisi ya Cyangugu. Sasa hivi si padri wetu hufanya mambo yake huru anapoishi uhamishoni”.

Jitihada zake za kushindania uongozi ziridhihirishwa kupitia kwa utando wa tuvuti wake leprophete.fr ambao hushutumiwa kusambaza habari za uchuki na uhamasishaji kuhusu utengano.

Habari kwenye ukurasa wa chama cha siasa Ishema ambacho huongozwa na mwenyewe Nahimana Thomas wamethibitisha habari za kurudi kwake nchini Rwanda na kushindania uongozi wa nchi.

[ad id=”72″]

“Bwana Padri Thomas Nahimana ambaye ni katibu mkuu wa chama ‘Ishema ry’u Rwanda’ pamoja na mshindani katika uchaguzi wa 2017 wa rais wa Rwanda; pamoja na kundi lake watatoka barani Ulaya leo jioni kwenye uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle nchini Ufaransa.”

Alipokuwa katika maongezi na waandishi wa habari mnamo tarehe 17 Novemba 2016 mjini Brussels nchini Ubelijiji, Nahimana alithibitisha jitihada zake za kurudi kwa nchi ya kizazi kutoka uhamishoni yaani nchini Ufaransa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.