kwamamaza 7

Mwanasheria Miguna Miguna awakosoa marais Kenyatta na Kagame “ Ni dharau kuzungumza masuala ya Afrika nchini Canada”

0

Mwanasheria asili ya Kenya Miguna Miguna amewakosoa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame  juu ya kujadiliana masuala yanayoihusu Afrika nchini Canada.

Miguna Miguna ameandika kwenye ukuta wake wa twitter kwamba mikutano ya namna hii ni dharau na ni ya kizamani.

“Jambo hili ni la kizamani.Viongozi wa Afrika kukutana kwa kuwa kusalimiana,kukumbatiana huko Ulaya na Marekani kaskazini baada ya kualikwa na serikali zinazolenga kuiba madini na mafuta barani Afrika” Miguna Miguna amepinga

Taarifa za Kenyans.co.ke huyu mwanasheria amemnyoshea kidole Uhuru Kenyatta kwamba anatumia ovyo mali ya umma.

“Unatumia Kshs miliyoni 200 kuwakuta Rais Kagame na Macky Sall badala ya kuwakuta Nairobi, Kigali ama Dakar? Acha matumizi mabaya ya mali. Acha ubabe kwa wakazi. Mkutane na kuhojiana masuala ya Afrika barani Afrika” ameongeza

Marais Kenyatta,Kagame na Macky wakizungumza nchini Canada/Picha na twitter

Miguna Miguna amefunguka haya baada ya Rais Kenyatta kuandika kwenye twitter kuwa amewakuta marais wenzake wakiwemo kabla ya mkutano wa G7.

Miguna Miguna ni mwanasiasa kiongozi wa NRM-K ambaye alizuia kurudi nchini Kenya baada ya kumuapisha mpinzani Raila Odinga.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.