kwamamaza 7

Mwanamke auawa na mamba akiwa anatafuta maji kwenye mto Nyabarongo

0

Mwanamke anayetambulika kwa jina la Nyirampakaniye Sperata raia wa Nyarugenge auawa na mamba akiwa amekwenda kuchota maji kwenye mto wa Nyabarongo ambao unapitia makazi yake kwenye tarafa ya Mageragere.

Meya wa wilaya ya Nyarugenge alithibitisha mkasa huu wa kifo cha Nyirampakaniye Sperata ikiwa kumekuwa na mpango wakuasilisha maji kwa wakazi wa eneo hili la Kavumu kulingana na taarifa hii iliyotangazwa na tovuti ya Igihe.com.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Tumekuwa na mpango wa kusambaza maji safi katika tarafa yote ya Mageragere mwaka, wakazi wa Nyarufunzo wana maji safi lakini wa Kavumu hawakuwa wajapata”

Bi huyu amekuwa akiishi eneo hilo la Kavumu ambalo halijafikiwa na maji.

Shirika la kusambaza maji likishirikiana na mamlaka ya wilaya ya Nyarugenge limeanza mfumo wa kusambaza maji kwenye karibu ya makazi ya wananchi. Alisema pia kwamba eneo hilo liko mahali yenye umbali mkubwa na kwa hivyo haiko rahisi kuasilisha maji hapo ila juhudi za kufikisha maji hapo zingali zinaendelea.

Bi huyu afariki saa za asubuhi mnamo saa 6h 30 akiwa anajitayarisha kwenda kanisa. Maiti yake yapelekwa hospitali kufanyiwa mitihani muhimu.

Ingawa serikali ya Rwanda imepiga hatua kwa kusambaza maji karibu na makazi ya wananchi kuna mahali ambayo ingali tatizo kubwa kupata maji na wanalazimika kufanya safari ndefu wakienda kutafuta maji. Kuna mpango wa kuvijenga viwanda kama Rukara II ambavyo vinatarajiwa kuondoa tatizo hili la maji.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.