kwamamaza 7

Mutenderi : Watoto wanaomba walio husika na mauaji ya Kimbari nao kutoa ushuhuda

0

Katika tendo la kuwakumbuka walio uawa katika mauaji ya Kimabri dhidi ya Watusi katika tarafa ya Mutenderi tarehe 17 April 2017, watoto walio zaliwa baada ya mauaji ya Kimbari waliomba walio husika na mauaji kutoa nao ushuhuda.

Vijana wa tarafa ya Mutenderi wanasema ya kuwa wanasikitishwa na kuwaona walio husika na mauaji ya Kimbari dhidi ya Watusi mwaka 1994, au jamii yao kutotoa ushuhuda na kusema jinsi mauaji yalifanyika, wanaona kuomba masamaha haitoshi, wanasema ingelikua vema pia wakisema maandalio ya mauaji.

Rutaganda Pacifique wa umri wa miaka 16 pamoja na wenzake wanasikitika kuwaona wahusika na mauaji ya Kimbari wakinyamaza kimya bila kutoa ushuhuda na wakijua mengi kuliko wanusra, kwa sababu wakisema jinsi ya mauaji yaweza kuwasaidia wengi kwa ajili ya umoja na kujua historia.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wanusra wa mauaji ya Kimbari katika tarafa hio nao huhakikisha kwamba wakati wa ukumbusho ni vema washuhuda wawe kwa ngazi mbili, muhusika na munusra kama vile husema ingufu.com.

Katika kumbukumbu la ukumbusho la Mutenderi kuna miili ya watu 4104 kutoka tarafa ya Ghara, Mutenderi pamoja na Kazo

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.