Swahili
Home » Musanze:Maseneta wawalaumu viongozi  juu ya ripoti zenye uongo”Gutekinika”
HABARI MPYA

Musanze:Maseneta wawalaumu viongozi  juu ya ripoti zenye uongo”Gutekinika”

Kwenye ziara yao ya kikazi wilayani Musanze,Maseneta  wamewalaumu viongozi wa wilaya hii  “gutekinika”yaani kudanganya takwimu kuhusu utekelezaji wa mipango ya serikali.

Mmoja mwa  hawa maseneta, Consolee Uwimana amemuuliza makamu wa kiongozi wa wilaya namna ambavyo viongozi wanaweza kueleza kufika utekelezaji wa kutoa maji  kiwango cha asilimia 89 wakati ambapo  kuna wakazi wanaokabiliana na funza.

“Mhe.makamu wa kiongozi wa wilaya ninatembea mala nyingi wilayani humu.Najua pengi penye funza, uktaka naweza kutaja,unaniambiaje kuwa mlitimza asilimia 89”amesema

Maseneta wameshangaa wakipofika tarafani Nkotsi ambako wakazi wanakabiliana  na ukosefu wa maji wakati wa miaka mitatu wakiwa na matanka ya maji matupu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Seneta Prof.Emmanuel Bajyana  Uwimana amesema kuwa suala hili ndilo chanzo cha malalamishi ya viongozi wa wilaya kusema kwamba bajeti haikutosha.

“Mnatuambia kuwa bajeti ilikuwa chache lakini hili hutokana na kuwa nyinyi mnatuambia kuwa hamna mengi ya kufanya mnapotuambiakuwa mlitekeza asilimia 89 au 95.Mnafikiri nani atawasidia?”ameuliza

Pengine Gavana wa mkoa wa kaskazini,Jean Marie Vianney Gatabazi amehakikisha kuwa viongozi wa wilaya mkoani wana tabia hii ya kudanganya takwimu za utekelezaji  wa mipango ya serikali

[xyz-ihs snippet=”google”]

Bw Gatabazi ametoa mfano wailaya ya Gicumbi iliyowahi kusema kuwa maji safi yaliwafikia wakazi  kiwango cha asilimia 80 wakati ambapo utekelezaji wa hili ulikuwa asilimia 40 tu.

Pamoja na hili,Waziri mkuu Dkt.Edouard Ngirente alipokuwa kwenye “Umwiherero” aliwataka viongozi kuacha tabia ya kutoa ripoti zenye uongo kwa kuwa zinazuia utekelezaji kamili wa mipango ya serikali.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com