kwamamaza 7

Muimbaji Kizito Mihigo aitaka mahakama kutoambatanisha kesi yake na ya mtangazaji Cassien Ntamuhanga

0

Muimbaji Kizito Mihigo  leo tarehe 14 Meyi 2018  amefikishwa mahakamani ya juu na kuitaka mahakama kutoambatanisha kesi yake na ya mtangazaji Cassien Ntamuhanga aliyetoroka gereza ya Mpanga.

Mshitakiwa ametoa ombi hili baada ya jaji kueleza kuna kizuzi cha kuwa  Cassien Ntamuhanga ambaye anashtakiwa pamoja na Kizito kwenye kesi hii alitoroka.

Kizito ameelezea jaji  kesi yake haina uhusiano wowote na ile ya Ntamuhanga kwani yeye anakubali kuwa na hatia kinyume na Ntamuhanga anayelaani mashtaka yote.

Mwanasheria wake, Me Mukamusoni amesema kesi ya mteja wake inastahili kutoambatanishwa na ya mshitakiwa aliyetoroka.

“Kwa upande wetu,tulingoja hii siku kwa hamu,tunahitaji haki”

Mahakama imepiga marufuku ombi la Kizito  kwa kusema kuna uhusiano kati yake na ile ya Ntamuhanga.

Kesi hii itaendelea tarehe 11 Juni 2018.

Kizito Mihigo alihukumiwa kufungwa miaka kumi jelani mwaka 2015 juu ya uhalifu wa usaliti,uundaji wa kundi la wanamgambo na kulenga kumfanyia maovu Rais Kagame.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.