kwamamaza 7

Muijiza! Mtoto wa kike mwenye umri wa miezi 7 aliyenusurika na ajali kali

0

Mtoto wa Kike alienusurika ajali kali kwa kutupiwa na mamake nje ya dirisha arudishwa nyumbani baada ya kupata matibabu.kwenye hospitali ya CHK.

 Mtoto huu anaeitwa Roxanne Abayizera amerudishwa nyumbani jumatano hii kutoka Hospitali ya CHUK baada ya kupona majeraha alioyapata kutokana na ajali hiyo ambayo ilisababisha vifo vya watu 14.

Roxanne Abayizera yuhu alinusurika ajali hii baada ya kutupiwa nje na mamake aliekuwa akikaa karibu na dirisha. Hii ilitokea baada ya gari la Kampuni ya huduma za kusafirisha watu ya Kigali Safaris kugongana na gari la aina ya Toyota Hilux na kupoteza barabara na kisha ikapinduka pinduka msituni chini ya kilima cha Shyorongi kilichopo taarafani Kanyinya wilayani NYARUGENGE.

Ange Uwamariya aliekuwa akihudumia mtoto huyo alisema kuwa mama huyo aliwaza kwamba mtoto huo angeweza kunusurika baada ya kumuona kijana mmoja akiruka kupitia dirisha na kumtupa nje na kwa bahati mtoto huo hakufariki .Ingawa alipata majeruhi ya viungo mbalimbai vya mwili vikiwemo mguu wa kushoto, kichwa na hata shingoni aliweza kupona baada ya kutibiwa na hospitali ya CHUK.

Polisi ilaarifu kwamba katika ajali hii ya gari la aina ya coaster iliyotokea majira ya saa saba jumamosi, tarehe 27 Mei 2017 waliyokuwemo watu wapatao 28, ilisababisha vifo vya watu 14 wakiwemo wanawake watano, wanaume saba na watoto wawili.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy/src.umuseke

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.