kwamamaza 7

Muhima: Imeonekana maiti ya kijana mwenye umri wa miaka karibu 25

0

Juma inne tarehe 14 Mach 2017 katika kiini ya Ubumwe, tarafa ya Muhima panapo julikana kwa jina la “Saint Famille” waliokota maiti ya kijana mwenye umri karibu miaka 25 ikifikiliwa kuwa aliuawa na polisi imeanza upelelezi ili kujua chanzo cha kifo hicho.

Wapita njia walio muona marehemu walisema ya kuwa walimuona karibu saa kumi na moja asubui na wamehakikisha kuwa sehemu hio huwa maibobo wengi wanao tumia dawa za kulevya.

Raia mmoja eti “barabara hii munaona, kati ya saa tisa na saa tisa na nusu kunakuwa wizi wengi sana wanakushika na wanakupiga. Hii si mara ya kwanza wanapiga mtu, ni tabia ya siku nyingi”.

Msemaji wa polisi mjini Kigali, Spt. Emmanuel Hitayezu, amesema ya kuwa wameanza upelelezi ili kujua sababisho la mpango huo mbovu.

Spt Hitayezu eti: « hadi sasa hatuja fahamu majina yake na tumeanza upelelezi na uchunguzi kwa kufahamu chanzo cha kifo hicho ».

[xyz-ihs snippet=”google”]

Msemaji wa polisi aliendelea na kusema ya kuwa usalama wa raia unazingatiwa tena ngazi za usalama na msingi ziko na ushirikiano wa usalama wa raia na mambo yao na ndio sababu sehemu tofauti huwa na makundi ya kulinda usalama katika vijiji na wanaomba wakaaji kutoa taarifa wakati wanafikiliwa uhalibifu wa usalama ili kuzuia makosa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.