kwamamaza 7

Muhanga:Viongozi wapatanisha raia na katibu mtendaji aliyeharibu chakula cha harusi.

0

Uongozi wa wilaya ya Muhanga wapatanisha mwenyeji  Minani Sylvestre na katibu mtendaji wa kijiji cha Kinini,tarafa ya Shyogwe aliyetupa chakula cha harusi kwa kuwa washiriki wa karamu hiyo hawakuhudhuria kampeni za uchaguzi.

Kitendo hiki bora kimetimizwa na kundi la viongozi  wa wilaya ya Muhanga akiwemo kiongozi mkuu wa wilaya,kiongozi makamu kwa wajibu wa uchumi na maendeleo,Katibu mtendaji wa tarafa la Shyogwe na wengi  walioshiriki katika harusi wameungana mikono ili kupatanisha  Minani na kiongozi wake Uwimana Fotide na kumshauri mengi kuhusu uongozi.Akisema kuhusu jambo hili,Minani amesema kuwa ameisha mpatia msamaa na kusema”Aliniambia kuwa hakuhusudia kuniudhi,ilikuwa kama ajali,nimeisha mpa msamaha”.

Kwa upande wake Uwimana Fotide ameomba msamaha familia ya Minani na kusema kuwa anakubai hatia ya kuingia nyumani kwake na kuzusha ghasia wakihofu kupigwa picha na kukimbia na ndipo chanzo cha kumwagika vinywaji na chakula walichoandaliwa.

Kiongozi wa Wilaya ya Muhanga,Uwamariya Beatrice yaeleza kuwa lengo lao si kupatanisha baali ni kuchunguza kuwa waliyoyasikia kuwa yaliyokea.Beatrice ameongeza kuwa tukio hili siyo gumu sana na kuzagaa kwake ni kutokana na wanaomchukia Uwimana Fotide waliondelea kusambaza maneno.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hili ni jambo lililotokea Mwezi July wakati amabapo Minani Sylivestre alikuwa na karamu nyumbani kwake,wakati wa kukaribisha wageni wake kwa chakula na vinywaji ndipo katibu mtendaji wa kijiji,Uwimana Fotide kuja  na watu  wakaanza kukimbia kisigino kisogoni.Ghasia ilizuka hapo hapo na wengi wakijiuliza kwa nini anakuja kuwatesa kwa kujifanya hajui kuwa kuwa kuhudhuria zile kampeni za uchaguzi ilikuwa ni hiari ya mtu pekee.

Mzee Minani Sylivestre  alisema kuwa kitendo cha kiongozi huyu kilimhuzunisha sana lakini kumuona kiongozi wake akija kumuomba msamaha ni jambo lililolahisisha mzigo aliokuwa nao moyoni mwake.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.