kwamamaza 7

Muhanga: Jeanne anadaiwa wizi wa watoto wawili

0

Nahabaramutse Jeanne mwenye umri wa miaka 22 amekamatwa na polisi kwa madai ya kuwaiba watoto wawili. Jeanne kutoka wilayani Muhanga alikubali kosa kwamba  ametumwa na mamake mdogo.

Mama yake mdogo alimpatia ujumbe kuwa anahitaji mtoto, kisha akamuomba kutafuta mtoto. Nahabaramutse Jeanne alielekea wilayani Rwamagana, alipoiba mtoto baada ya kumpewa na mamake (Mzazi wa mtoto) wakati wa kuenda haja kubwa.

[ad id=”72″]

“Mama mdogo aliniambai kuiba mtoto, najuta kwani sikumuambia kiongozi yoyote.” Jeanne alieleza.

Daria Uwizeye ambaye ni mzazi wa mtoto aliyeibiwa wilayani Rwamagana, alieleza kwamba alienda sokoni pamoja na jambazi la watoto (Nahabaramutse Jeanne) na walipofika karibu na soko akampatia mtoto ili kujisaidia; aliporudi hakumkuta jambazi huo na wenzake wakamuambia kuwa ameisha pata pikipiki.

Daria akieleza yaliyofuata baada ya kukosa mtoto wake alisema, “Niliwaambia polisi ili kutafuta, waliniita baadaye kwamba mhukumiwa amekamatiwa katika wilaya ya Muhanga baada ya mwezi mzima na wiki mbili bila kumkuta mtoto wangu.”

[ad id=”72″]

Raia walioshirika katika kukamatwa kwake, husema kwamba Jeanne aliwadanganya kuwa mtoto huo ni wake. Aliwahi kuiba mtoto mwingine, lakini alimtupa mwituni baada ya kugunduliwa na raia pamoja na shirika za usalama.

Nahabaramutse Jeanne amefungiwa katika kituo cha polisi cha Kiyumba. Mahakamani alikubali kosa la wizi wa mtoto na kuomba msamaha.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.