Home HABARI Muhanga: Aliyemuua mwendesha pipipiki atakiwa kifungo cha maisha jela
HABARI - June 27, 2017

Muhanga: Aliyemuua mwendesha pipipiki atakiwa kifungo cha maisha jela

Undeshaji mashtaka wamtakia, Niyibigira Bruce, Kijana mwenye umri wa miaka 24 aneyeshitakiwa kwa kumuua mwendesha pikipiki baada ya kumchoma visu akijaribu kuiba pikipiki.

Katika mwisho wa wiki jana, tarehe 22 Juni ndipo uendeshaji mashtaka, Wa Ngazi ya Juu ya Muhanga, ulipomtakia kifungo cha maisha jela kulingana na uzito wa hatia anoyoshtakiwa.

Kijana huu anayeshtakiwa kupanga njama za kumuua mwendesha pikipiki anayetambulika kwa jina la Twagirimana Gabriel akikusudia kumuiba pikipiki yake, alipanga njama na mtu anayesema anaitwa Gataje ambaye alichukua pikipiki hiyi na kumufikisha mahali walipopanga na Niyibigira.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Alipofika hapo , Gataje, alimwomba mwendesha pikipiki kusimama na hapo Niyibigira alijitokeza kutoka mahali alipokuwa amejificha na kumuvamia kwa kumuchoma visu Twagirimana,alipojaribu kujilinda kwa nguvu walimchoma kisu kingine kifuani hadi alipofariki.

Kulingana na habari hii ya Uendeshaji mashtaka wa Juu zaidi, baada ya kumuua mwendeshaji pikipiki Niyibigira, alimvua nguo, na kuchukua vitambulisho vyake na hata vyeti vya pikipiki hiyo, alipojaribu kukimbia raia wengine walikimbizana naye hadi walipomkamata.

Gataje naye alijaribu kuichukua pikipiki hiyo na kushindwa kwa sababu wakazi wa hapo walikuwa wakiwakimbizana, na aliiacha na kukimbia, mpaka sasa hakuna anayejua mahali alipo.

Mara baada ya kukamatwa alikiri mashtaka, na kuongeza kwamba hii si mara ya kwanza kwake kufanya uhalifu kama huyu kwa kuwa mwezi Disemba wa 2016 alimuua mwendesha pikipiki mwingine na kumnyanganya pikipiki yake na kwenda kuiuza.

Uamuzi wa kesi huu unatarajiwa kusomwa tarehe hii ya 27 Juni 2017 saa Kumi. Na huenda akahukumiwa kifungo cha maisha gerezani kulingana na ibara la 140 la kanuni ya Adhabu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.