kwamamaza 7

“Muambiye raia wa Rwanda kua mfalme mwengine ameteuliwa kuchukua na fasi ya Kigeli V Ndahindurwa” Benzige Boniface

0

[ad id=”72″]

Wakati mwili wa marehemu mfalme  Kigeli V Ndahindurwa kufika Rwanda, wafuasi wake pakiwemo katibu wake Boniface Benzige walikua wakifikiriya atakaye chukuwa fasi ya ufalme na hasa tayari ametangazwa ijapo kuwa kuna mila nyingine watakazo zifuata.

Mdogo yake marehemu mfalme Kigeli V Ndahindurwa aitwaye Bushayija Emmanuel ndiye aliyetangazwa kuwa mteule wa ufalme wa Rwanda, na huyu Benzige hakusema nafasi huyu mfalme alipoteuliwa kwa ajili ya usalama wa wafuasi wake.

Benzige eti “Nawashukuru, kwa niaba yetu muwambiye wanyarwanda kuwa ameteuliwa mfalme mwengine, na atakuwa akikubaliwa na sheria, na tutakapo maliza mila na desturi za lazima, atatoa neni, ila tulipenda kuwajulisha kama wanyarwanda wapo na mfalme “.

Huyu aliyeteuliwa alizaliwa mwaka wa 1960, baba mzazi ni Bushayija wa Yuhi Musinga, atachukua jina la kiufalme la Yuhi VI kwani kizazi cheke kilikua Yuhi wa Tatu aliyezaliwa pamoja na mfalme aliye fariki.

Mfalme Kigeli v alifariki akiwa katika taifa lingine, na huyu aliteuliwa, ameteuliwa akiwa nafasi isiyojulikana nje ya Rwanda, hayo ni kama michezo, wafalme hao husema ni wafalme wa Rwanda ijapokua ulimwengu wote na umoja wa mataifa hujua kuwa Rwanda huongozwa kama Jamhuri.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.