Home BIASHARA Mswada wa sheria ya mkopo wa billion 75 £ za kujenga barabara ya Nyanza- Ngoma wapitishwa
BIASHARA - HABARI - August 9, 2017

Mswada wa sheria ya mkopo wa billion 75 £ za kujenga barabara ya Nyanza- Ngoma wapitishwa

Bunge la Rwanda imepitisha mswada wa sheria ya mkopo kati ya serikali ya Rwanda na shirika la IDA  kuijenga barabara ambayo itatoka wilaya ya Ngoma kupitia Rwamagana na Bugesera  hadi Nyanza .

Mswada huu  wa mkopo wa milioni 75£ni sehemu ya mradi wa uchukuzi katika ziwa Victoria lakini mradi mwenye utahusishwa na kuijenga barabara hii ya mwendo wa kilomita 119.

Alipokuwa akifafanua mbele ya bunge kuhusu mswada huu, Waziri wa Mipango na Uchumi Balozi Gatete Claver amesema kwamba mkopo huu utasaidia kuimarisha sera za serikali za miundombinu.

Alieleza kwamba fedha hizi zitatumiwa kujenga sehemu moja ya barabara hii ambako fedha nyingine zitatolewa na nchi ya Ujapani.

Barabara hii ni mojawapo ya maahidi ya Rais Kagame kwa wananchi wa Ngoma ambapo aliwaambia barabara kubwa ambayo itawaunganisha na wilaya ya Nyanza itajengwa kwenye siku za hivi karibuni.

Makubaliano ya mkopo kati ya serikali ya Rwanda na Benki ya Dunia yalipigiwa sahihi na waziri Balozi Claver Gatete na msimamizi wa Benki ya Dunia nchini Rwanda Yasser –El Gammal.

Barabara hii ambayo itaanza kujengwa mwishoni mwaka huu, inatarajiwa kuleta manufaa kadhaa kwa wananchi kwa kuwa watakuwa na fursa ya kuanza biashara mpya  zitakazowasaidia kujikwamua na umaskini na wengine wataweza kuajiriwa kupitia ujenzi wa barabara hii. Pengine itasaidia kuimarisha shughuli za uchukuzi na kupunguza mlolongo wa magari yaliyokuwa yakitumia barabara ya Rusumo-Kigali.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.