kwamamaza 7

Mshitakiwa wa kumteka nyara mrinzi wa Rais Kagame apigia mayowe Umoja wa Mataifa

0

 

Familia ya mshitakiwa wa kumteka nyara aliyekuwa mrinzi wa Rais Kagame Luteni Joel Mutabazi,Rene Rutagungira  imeandikia barua Umoja wa Mataifa(YUNA) idhaa ya haki za binadamu nchini Uganda ikidai  huyu mfungwa anafanyiwa utesaji wa kimwili gerezani.

Wanafamilia wake tarehe 9 Mei 2018 kupitia wanasheria wake Kiiza na Mugisha waliandika  hivi vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinafanywa na maafisa wa usalama wa Uganda.

Dailymonitor nchini Uganda imeandika barua hii ilieleza tangu alipokamatwa mwaka 2017,Rutagungira alifanyiwa utesaji wa kimwili na kimantiki kama vile kufungwa kiupweke.

Familia yake imependekeza  mambo ya ukiukaji wa haki za Rutagungira kukomeshwa  pamoja na kumruhusu kutembelewa na wanafamilia yake.

Rene Rutagungira alikamatwa na maafisa wa upelelezi wa Uganda(CMI) akiwa pamoja na maafisa tisa wa polisi nchini Uganda.

Hawa walishtakiwa kumteka nyara na kumrudisha nchini Rwanda aliyekuwa mrinzi wa Rais Kagame,Luteni Joel Mutabazi.Hata hivyo,serikali ya Rwanda kupitia msemaji wa Polisi CP Theos Badege alisema jambo hili lilifuatwa sheria za kimataifa

Luteni Joel Mutabazi alihukumiwa  kufungwa maisha jela na mahakama za kijeshi nchini Rwanda mwaka 2014.Alishtakiwa ushirikiano na FDLR na RNC ili kuharibu usalama wa nchi na mauaji.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.