kwamamaza 7

Mrithi wa marehemu Mowzey Radio kujulikana

0

Familia ya marehehemu muimbaji Moses Ssekibogo Nakitinje maarufu kama Mowzey Radio inatarajia kumuweka wazi mrithi wa mali ya marehemu.

Mmoja mwa familia ya Mowzey Radio ametangaza familia yao inajianda vilivyo kuelekea alipozikwa Radio eneo la Nakawuka Kagga mjini Kampala kwa kumuomboleza marehemu kabla ya kutangaza mrithi.

Tutakwenda kule Nakawuka jumatano ilikufanya maandalizi,tukakuwa kule siku ya alhamisi,ijumaa na jumamosi,tutarudi mjini Kampala baada ya kumchagua mrithi”ametangazia Ugblizz.

Bin Mowzey Radio,Ayana Ssekibogo Kazooba akimlilia baba yake/Picha na ugblizz.

Huyu ameongeza kwamba wanafikiri kuwa bin Radio Asante ndiye atakayechaguliwa lakini familia itaamua kivyake.

Isisahaulike kwamba kutoelewana kulizuka baada ya siku 17 za kifo cha Radio kati ya ami yake Frank Ssekibogo na Balaam juu ya kuiba fedha zilizotolewa kwenye msiba wa marehemu pamoja na tukio la aliyewahi kuwa meneja wa Goodlyfe Jeff Kiwanuka kutangaza kwamba anamiliki  nusu jumba ya Neverland.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Inatarajika kwamba mrithi atachaguliwa miongoni mwa watoto watatu;wavulana wawili na msichana mmoja aliyemzaa na muimbaji Lilian Mbabazi.

Muimbaji Mowzey Radio aliaga dunia tarehe mosi Februari 2018 baada ya kupigwa alipokuwa baani De Bar eneo la Entebbe,35Km kutoka Kampala.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.