kwamamaza 7

Mpinzani mkubwa nchini Rwanda aachiwa huru

0

Mpinzani wa serikali nchini Rwanda, Ingabire Victoire Umuhoza ameachiwa huru.

Tangazo la Wizara ya Haki la jana tarehe 15 Septemba linaeleza huyu ameachiwa huru kufuatia sheria (Law No. 30/2013 of 24/5/2013) husika na hukumu ya uhalifu nchini  makala yake 245 na 246 husika na  kufunguliwa mapema.

Umuzi huu pia unahusu katiba ya nchi katika makala yake ya 109 kwamba Rais ana uwezo wa kumuachia huru mfungwa kufuatia sheria baada ya kuhojiana na Mahakama kuu nchini.

Pia ni kulingana na ombi lake Ingabire mwezi Juni, jambo ambalo wanachama wake wamekanusha katika mazungumzo na Sauti ya Marekani.

Mwingine ambaye ameachiwa huru ni muimbaji gwiji, Kizito Mihigo ambaye alifungwa mwaka 2014 juu ya usaliti kwa  nchi.

Ingabire Victoire ni Mwenyekiti na Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Rwanda kwa jina la FDU-Inkingi ambacho hakijasaljiliwa rasmi.

Alifungwa mwaka 2013 juu ya mashtaka ya kuwa na itikadi ya mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi 1994 na kuwa kizuizi kwa usalama wa nchi.

Wafungwa 2,138 pia wameachiwa huru kwa masamaha wa Rais Kagame.

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.