Swahili
Home » Mpayimana yakubali matokeo ya kura baada ya rais Kagame kuwapiku kwa kishindo
HABARI

Mpayimana yakubali matokeo ya kura baada ya rais Kagame kuwapiku kwa kishindo

Mgombea urais wa kujitegemea Mpayimana Philippe ambaye alikuwa ndiye mgombea huru pekee katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana tarehe 4 Agosti.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mpayimana sawa na Frank Habineza hawakuweza kupata hata asilimia 1 ya kura baada ya tume ya uchaguzi wa Rwanda kutangaza asilimia 80 ya matokeo ya kura kwa ujumla.

Mpayimana ambaye amekuwa akifuatia matokeo ya kura kutoka hoteli ya Capri iliyoko Nyamirambo wilaya ya Nyarugenge.

Ametoa hutuba yake kwenye lugha tatu, Kifaransa, Kingereza na Kinyarwanda amesema kwamba anafurahia zoezi nzima ya kura na kwamba anaheshimu matakwa ya wananchi wa Rwanda.

“nawashukuru viongozi wa ngazi za nchi za nchi ambao walinisaidia kuendesha kampeni zangu mbali na pingamizi nilizozikuta hapo wiki ya kwanza. Nchi yetu iliimarika kiusalama na kidemokrasi”Asema.

Akiulizwa ikiwa aliwahi kulifikia lengo lake, alisema kwamba alikwishalifikia lengo lake

“nimewahi kuihamasisha demokrasi na nitaendelea na mipango yangu ya kisiasa ikiwa kuna yeyote anayependa kujiunga aje tushirikiane”

Aliwapa moyo waungamukono wake kwamba hawana sababu ya kupuuza idadi ya kura walizozipata na kuwaambia kwamba na hata sauti za wachache zinasikiwa na kwamba wataweza kuzitumia kwa kutekeleza mipango yao ya kisiasa.

Sera za mgombea Mpayimana Philippe zilikuwemo kuimarisha demokrasi, biashara, na kilimo na hata kutia mkazo maendeleo ya vijana.

Hata hivyo mgombea mwingine, Frank Habineza, hakuzungumza na vyombo vya habari kwa  kueleza kwamba atakuwa na mahojiano nao baada ya matokeo ya kura kutolewa.

Habineza amekuwa akingojea matokeo ya kura kupitia vyombo vya habari vya taifa kwenye hoteli ya Lemigo akiwa na familia yake ambako aliwapokea waandishi wa habari kwa chakula cha jioni.

Matokeo ya kura ya muda yaliyotolewa na tume ya uchaguzi kupitia asilimia 80 ya jumla ya kura yanaonyesha kwamba Paul Kagame amekwisha jipatia ushindi mnono wa asilimia 98.66 akifuatiwa na Mpayimana Philippe na asilimia 0.72 halafu  Habineza Frank na asilimia 0.42.

Matokeo mengine yatatolewa jioni hii baada ya kupokea kura kutoka wilaya zote.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com