kwamamaza 7

Mpango gani wa serikali kuhusu wabadhirifu wa mradi wa kuwapatia ng’ombe raia ‘Girinka’?

0

Serikali ya Rwanda ilianzisha mradi wa kuwapatia ng’ombe raia maskini katika mradi ulistahiliwa ‘Girinka’ maana yake kuwa na ng’ombe. Mradi huu ulianza mnamo mwaka wa 2006, ijapokuwa viongozi wengi wa mitaa walidaiwa kuwanyanganya raia ng’ombe wangepatiwa.

Mradi wa ‘Girinka’ ulikabiliwa na ubadhirifu wa viongozi wanaowapatia ng’ombe watu Fulani badala ya wasiojiweza. Wengi walipigwa jela kwa ajili ya ubadhirifu na wengine kwa kuomba rushwa raia maskini kabla ya kuwekwa kwenye orodha ya wafadhiliwa.

[ad id=”72″]

Bodi ya kilimo nchini Rwanda (RAB) ilisema kwamba zaidi ya ng’ombe 729 walipotelea na wengine zaidi 614 walipatiwa raia ambao hawafai kupewa ng’ombe wa maskini.

dr_mark_cyubahiro_bagabe_
Kiongozi mkuu wa RAB, Dkt Mark Cyubahiro Bagabe

Kiongozi mkuu wa RAB, Dkt Mark Cyubahiro Bagabe akisema kuhusu habari zilisambazwa na raia kwamba viongozi wa mitaa walijipatia ng’ombe pekee; alisema kwamba serikali haitawasamehe wabadhirifu wa mradi huu.

Cyubahiro alisema, “Si kazi rahisi kuwagunduwa wote walitumia ulafi na ujanja katika mradi huu kwa raia, lakini serikali ya Rwanda inaendelea kukabiliana nao.”

Mradi wa ‘Girinka’uliwanufaisha raia; zaidi ya ng’ombe 253,354 walipewa wananchi maskini. Inatarajiwa kwamba mnamo mwaka wa 2017 wafadhiliwa zaidi ya 350,000 watanufaishwa na mradi wa Girinka.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.