kwamamaza 7

Mnyarwanda mwingine atekwa nyara nchini Uganda

0

Mnyarwanda kwa jina la Claude Iyakaremye alitoweka mjini Kampala jumapili baada ya watu wasiojulikana  kumuweka garini nambari UAJ 921 G kwa nguvu.

Bi Iyakaremye,Beatrice Nyirahabimana ametangazia Chimpreports kuwa mume wake alikamatwa alipokuwa kwenye kituo cha magari ya Volcano mjini Kampala

“ Nilijulisha kituo cha polisi cha Old Kampala jumatatu,walinishauri kuenda kwa Mkurugenzi wa Ofisi ya upelelezi wa kijeshi ili kuzua mengi zaidi” Beatrice amesema

Msemaji wa Polisi ya Uganda, Emillian Kayima  ameeleza lazima hili liulizwe msemaji wa jeshi, Brig. Richard Karemire.

“ Kama viongozi wetu wanavyosema,haina budi kujulisha uongozi husika,bila shaka suala hili litajadiliwa vilivyo”amesema Karemire.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kuna taarifa kwamba gari lililombeba  ni la maafisa wa usalama

Hili ni baada ya mazungumzo yaliyotokea juma pili kati ya  Rais wa Uganda,Yoweli Museveni na mwenzake  Kagame na kuamua kwamba masuala kama haya yanastahili unyenyekevu na thibitisho.

Isisahaulike kuwa  Wanyarwanda karibu 1,000 walikamatwa na kuteswa kimwili nchini Uganda kwa kutuhumiwa kuwa wapelelezi wa Rwanda.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.