Swahili
HABARI MPYA

Mnyarwanda atekwa nyara na watu wenye silaha mjini Kampala

Mnyarwanda kwa majina ya  Philip Rwakibibi jumanne wiki hii alikamatwa na watu wenye silaha wakidai ni maafisa wa usalama.

Kwa mujibu wa taarifa za Chimpreports shahidi wa hili tukio amesema Rwakibibi alianza  kupambana na hawa watu lakini wakamzidi nguvu kisha wakamtia garini la aina ya RAV 4 na kuenda zao.

“Tumeshangaa kuona wanaume kutoka garini na kumtaka Philip kuingia ndani” Amesema afisa wa kampuni ya Trinity Bus

“Hawa wanaume walimuambia ni maafisa wa usalama kisha wakatoa bunduki zao wakimbabisha watampia risasi. Kisha wakamtia garini” ameongeza

Bi Rwakibibi, Janeanette ameeleza ameambiwa alikolazwa hospitali kuwa mumewe amekamatwa na wanausalama.

“ Sijui walikompeleka na nimesononeka sana” Kwa kuongeza “ Hana uhusiano wowote na Jeshi ama usalama wa Rwanda”

Rwakibibi ambaye ni Mnyarwanda asili ya DR Congo ni mfanyakazi wa kawaida ambaye kazi yake ni kutia mizigo ya abiria katika magari kutoka Kampala-Goma.

Msemaji wa  jeshi nchini humo, Brig. Richard Karemire ametangaza hajui kuhusu hili tukio.

Pia Kiongozi wa Ofisi ya upelelezi wa kijeshi, Brig. Jen. ametangaza hayupo nchini.

Pamoja na hayo, Wanyarwanda walianza kukamatwa tangu mwaka 2017 kwa mashtaka ya kuwa wapelelezi wa Rwanda.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com