Swahili
HABARI MPYA

Mnyarwanda aliyetekwa nyara nchini Uganda aeleza alivyoteswa kimwili

Mnyarwanda Emmanuel  Cyemayire,44, alikamatwa na maafisa wa upelelezi wa Uganda,CMI tarehe 4 Januari mwaka 2018 na kuachiwa huru jana tarehe 29 Januari 2018 baada ya kunyanyaswa na kuteswa kimwili anapopaita “jahanamu”.

Akizungumza na vyombo vya habari leo mjni Kigali,Cyemayire ameeleza kwamba hajaamini kuwa amefika nchini Rwanda baada ya kupigwa usiku mchana,kufungiwa katika maji na mateso mengine ya kiunyama.

“Nafikiri kuwa ni ndoto,sijahakikisha kwamba nimefika,nimetoka jahanamu”amesema Cyemayire.

Bw Cyemayire ameeleza kwamba mwa waliomteka nyara  anamjua afisa wa upelelezi wa Uganda, Maj.Mushambo aliyempeleka kituo cha jeshi cha Makenke mjini Mbarara,mahali ambapo alimaliza siku nane kwa kufungwa mikono na miguu  yake ikining’inia.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Cyemayire ametangaza kuumia mgongo  juu ya kuteswa  kimwili.Huyu ni miongoni mwa Wanyarwanda waliokamatwa nchini Uganda ambao wanawashataki maafisa wa CMI kuwateka nyara na kuwatesa kimwili kwa kuwashtaki kuwa wapelelezi wa Rwanda.

Kwa upande mwingine,serikali ya Uganda ilijibu Rwanda kwamba Wanyarwanda wanaokamatwa ni wale ambao wanahusiana na vitendo vya ugaidi nchini Uganda.

Bonyeza BWIZA TV kupata habari  na nyimbo mpya

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com