kwamamaza 7

Mnada wa mali nyingine ya famlia ya Rwigara wahairishwa

0

Mnada wa mashine za kuandaa sigara za kiwanda Premier Tobacco cha familia ya Rwigara umehairishwa  baada ya familia ya Rwigara kutoa ombi la kutokubali bei iliyotolewa.

Mfanyakazi wa mahakama Me Vedaste Habimana ameeleza  kamati kuwa sheria zinakubalia familia ya Rwigara kutoa bei la mali yao kinyume na iliyotolewa na wale wa Bodi Kuu ya Kodi nchini Rwanda (RRA).

“ Mwanasheria wa PTC aliniandikia tarehe 9 Juni kwamba hawakubaliani na bei iliyotolewa,walisema kuwa wanatakakutoa bei yao. Sheria inakubalia pande zote mbili kupiga marufuku bei ya mali inayouzwa mnada”

RRA iliuza mnada  sigara iliyotengenezwa tarehe 28 Machi 2018 frw miliyoni 512.

Kwa sasa familia hii inawakirishwa na binti marehemu Assinapol Rwigara Adeline Rwigara baada ya bi Rwigara, Adeline Rwigara Mukangemanyi na binti ye Diane Rwigara Nshimiyimana kufungwa kwa kushtakiwa uchochezi,matumizi ya hati bandia.

Mala nyingi washtakiwa walilaani haya mashtaka kwa kusema kwamba ni ajili ya kisiasa na kuongeza hawana deni la frw biliyoni tano  kwa serikali ya Rwanda.

Kuna taarifa kwamba RRA ilitoa bei ya frw biliyoni 1.2

Mnada utaendelea tarehe 18 Juni 2018

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.