Swahili
Home » Mmoja mwa washiriki wa RNC ajiondoa na kuanzisha  chama chake cha upinzani kwa serikali ya Rwanda
HABARI SIASA

Mmoja mwa washiriki wa RNC ajiondoa na kuanzisha  chama chake cha upinzani kwa serikali ya Rwanda

Mwanamume kwa jina la Callixte Nsabimana anayejulikana kama Sankara ameanzisha chama chake, ‘Rwandese Revolutionary Movement (MRR) anachokita kuwa cha upinzani wa Rwanda baada ya wiki moja ya kujiondoa katika chama cha RNC.

Kupitia barua yake na  kwa mazungumzo kwenye radiyo moja ugenini,Sankara ametangaza kuwa aliamua kujioandoa katika RNC alipogundua kuwa chama hiki hakinaenda goigoi  kisiasa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kupitia mtandao wa facebook,Nsabimana ameandikia mkurugenzi wa chama cha RNC,mkoa wa Afrika kusini,David Batenga kuwa muda umefika wa kufanya analolifikiri kwa kuwa alikuwa akiona kwamba kanuni zilizomfanya kujiunga na RNC hazifuatiliwi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Callixte Nsabimana alikuwa mwanajeshi wa Rwanda mwenye cheo cha Sajinti kabla ya kutoroka na kuenda nchini Uingereza na alikuwa na nafasi ya wajibu wa utangazaji katika mkoa wa Afrika kusini wa RNC.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com