kwamamaza 7

Mkuu wa Jeshi la Rwanda awasili nchini DR Congo

0

Rais wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi amemkalibisha Mkuu wa Jeshi la Rwanda, Jen. Patrick Nyamvumba halafu wakazungmuza kuhusu ushirikiano wa jeshi la nchi mbili.

Baada ya mazungumzo, Jen. Nyamvumba amesema ziara yake ni ya kushuru ushirikiano mzuri ulioko kati ya Jeshi la Rwanda na DRC.

“ Tumekuja kumheshimu Tshisekedi na kushsukuru ushirikiano wa Jeshi la FARDC,”  Jen. Nyamvumba amesema

Mkuu wa Jeshi la DRC, Luteni Jenerali Célestin Mbala Munsense, amesema  majirani hawana budi kushirikiana kwa ajili ya amani.

“ Sisi ni majirani, na tunapaswa kuongeza ushirikiano kwa ajili ya amani katika eneo hili.” Jen. Munsense amesema

Ziara hii ni baada ya FARDC kuwakamata na kuwapeleka nchini Rwanda aliyekuwa Msemaji wa wanamgambo wa FDLR, Nkaka Ignace na Mkuu wa Upelelezi, Lt. Kanali, Abega.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.