kwamamaza 7

Mkuu wa jeshi la Burundi amuunga mkono Jenerali Kayumba Nyamwasa

0

Taarifa zimezagaa kwamba mkuu wa jeshi la Burundi,Jenerali Prime Niyongabo anamsadia mno mwenyekiti na kiongozi wa chama cha RNC,Jenerali Kayumba Faustin Nyamwasa katika mambo ya kurahisisha usafirishaji wa watu wanaosajiliwa kujiunga na jeshi la chama hiki huko kusini mashariki ya DR Cong,eneo la Minembwe.

Taarifa za chombo cha habari nchini Uganda,Virunga Post zimeeleza kuwa taarifa hizi zilihakikishwa na waliowahi kusajiliwa kujiunga na jeshi la RNC kutoka nchini Uganda.

Hawa walitangaza kwamba walitoka nchini Uganda na kuelekea nchini Burundi kisha wakasindikizwa na wanajeshi wa Burundi kwa msaada wa mkuu wa jeshi la Burundi, Jenerali Prime Niyongabo hadi walipovuka eneo la Minembwe,mahali ambapo kunasemekana kuwa ni kambi ya mafunzo ya jeshi la  RNC ya Jenerali Kayumba Nyamwasa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na hili, taarifa za chombo hiki zinasema kwamba mmoja mwa watangazaji wake aliweza kutupia jicho ripoti ya Umoja wa Mataifa(YUNA) isemayo kwamba baadhi ya waliosajiliwa na jeshi la RNC walijiuzulu na kuenda kwenye makao  ya MONUSCO eneo la Kivu ili kujadili namna za kurudi kwao nchini Rwanda.

Isisahaulike kwamba ushirikiano kati ya Rwanda na Uganda ni mkia wa mbuzi tangu mwaka 2015 baada ya Burundi kushtaki Rwanda kuwa chanzo cha kutaka kuipindua serikali ya Rais Nkurunziza.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.