Msichana mwenye umri wa miaka 16 kwa sasa yuko katika hali mbaya na anapewa matibabu kwenye kituo cha One Stop Center cha Kacyiru baada ya kuteswa akipigwa kiunyamana na kunyanyaswa na bosi mama wa nyumbani aliyekuwa anamtumikia.

Msichana huyu aliyesema kuwa ni kutoka wilaya ya Rulindo alifika hapa akija kufanya kazi mjini Kigali na mtu aliyemleta akampeleka moja kwa moja katika nyumba ya Bosi huyu mkatili.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Amesema kwamba amekuwa akimfungia nyumba na kumpiga kila siku kiunyama kwa kutumia nyuzi za umeme na hasa kwa makosa madogo sana katika mateso hayo aliyoyashuhudia kwa kipindi cha miezi 18.

Msichana huyu alisema kwamba alifika mnamo mwaka nusu iliyopita akija kuwalea watoto 2 wa bosi wake mama huyo na tangu wakati huo hakuweza kufika nje ya nyumba hiyo na alikuwa akikabili mateso yakiwemo kupigwa usiku na mchana.

alimokuwa akifungiwa

Mama huyu alikuwa akimpiga baada ya kumvua msichana huo nguo zote na kumpiga bila kujali sehemu za mwili.

Habari za kuwa Bosi mama huyo anamtesa mtumishi wake zilitolewa na majirani na hivyo ngazi za usalama zikajitokeza kumsaidia mtoto huyo na ilikuwa tarehe 19 Juni mwaka huyo.

Majirani wa mama huyo walisema kwamba jirani wao wamemzowea kwa vitendo vya kiunyama na alikuwa akiwafanyia maovu hayo watumishi wake waliomfanyia kazi.

Hivi sasa kesi ya kumtesa mtoto huo imekwishapelekwa mahakamani na katika uamuzi wake wa awali, mahakama ilikuwa imemhukumia kifungo cha miaka mitatu na faini ya laki tano za faranga za Rwanda kwa makosa ya kupiga na kujeruhi hata hivyo kesi hiyo huenda ikaendeshwa tena kwa kuwa ilipewa maani isiyofaa ambapo ingekuwa kitendo cha unyanyasaji wa kikatili.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.