kwamamaza 7

Mkute Dk. Frank Habineza aliyewahi kuwa mgombea wa urais mwaka 2017

0

Dk. Frank Habineza ni Mwanasiasa na mwanzilishi wa chama cha ‘Democratic Green Party of Rwanda’ kilichosajiliwa rasmi tarehe 9 Ogasti 2013.Alizaliwa Wilayani Mityana nchini Uganda tarehe 22 Februari  mwaka 1977.

Anamiliki shahada katika mambo ya Uongozi wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Rwanda (UNR) mwaka 2005 na shahada ya uzamili  katika mambo ya Sayansi katika siasa na Vita kutoka Chuo cha Usalama nchini Sweden. Pia ana shahada ya uzamivu kutoka Koleji ya Bethel-Indiana nchini Marekani.

Pia,Dr.Frank Habineza ni mtetezi wa mazingira,haki za binadamu demokrasia na mtaalamu wa mambo ya ulinzi na usalama.

Huyu alikuwa mgombea wa urais mwaka 2017 kwa niaba ya chama chake na aliongoza muungano unaoundwa na nchi 30 wa vyama vya kisiasa kwa jina la ‘African Greens Federation’wenye makao nchini Burkina Faso.

Anajulikana kwa uanzilishi wa shilika la kutetea mazingira kwa jina la ‘Rwanda Wildlife Clubs ’alipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka 1999. Baadaye,alikuwa mshauri pekee wa Waziri wa Ardhi,Mzingira,Maji na Madini mnamo mwaka 2005.

Dk.Frank Habineza aliwahi kuwa mwandishi wa vyombo vya habari kama vikiwemo UMUSESO,Rwanda Newsline na Rwanda Herald alipokuwa chuoni.

Kwa mamboi ya mazingira,huyu kiongozi alikuwa muunganishaji wa muungano wa ‘Nile Basin Discourse’ nchini Rwanda tangu mwaka 2006-2009.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song update

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.