Swahili
HABARI MPYA

Mkurugenzi wa Radiyo iliyofungwa na serikali ya #Rwanda wa afunguka kilichomfanya kukataa kuomba msamaha

Mkurugenzi wa Radiyo ya Amazing Grace Pastor Gregg Schoof amesema hakuomba msamaha kutokana na kuwa  anaona ni jambo kinyume na yale anayofokiri .

Pastor Gregg amewaambia watangazaji hakutii amri ya serikali kuomba msamaha baada ya ujumbe  wa kuwapinga wanawake ambao ulitolewa kupitia sitesheni yake.

Huyu amesema  hastahili kuomba msamaha kwani si yeye aliyesema maneno ya kupuuza wanawake

“sasa cha kwanza niliambia serikali mimi ni Pastor  Schoof siyo Pastor Nicholas.Siwezi kuomba msamaha kwa niaba ya mtu ambaye hana hatia.Haikutokea kesi mahakamani”

“Ikumbukwe kwamba Pastor  Nicholas alikuja kwenye rediyo na kueleza kuhusu hili jamb.Ina maana kwamba nikiomba msamaha nitakuwa na hatia”ameongeza.

Rediyo Amazing Grace ilifungwa jana tarehe 24 Aprili kupitia tangazo la serikali likieleza ilidharau amri ya serikali.

Amri ya serikali ilikuwa kuomba  msamaha,kulipa faini Frw miliyoni mbili na kuacha kazi zake  za kila siku mwezi mzima.

Mkurugenzi wa Radiyo Amazing Grace, Past. Gregg Schoof

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com