kwamamaza 7

Mkee wa rais aomba wazazi kuhifadhi haki za wanawake

0

Mkee wa rais Jeannette Kagame aliwaomba wazazi kuhifadhi haki za watoto hasahasa wa kike ili kujenga familia nzuri. Alitoa mwito jana 15 Oktoba 2016 alipokuwa wilayani Nyaruguru/Cyahinda katika sherehe za sikukuu ya kimataifa ya wanawake wa kijijini.

Bi Jeannette kagame aliwaambia wazazi kuwapatia watoto elimu ya kutosha na kuwasaidia watoto wa kike ili kujenga familia yenye matumaini ya kuwasaidia wasichana.

“Nyinyi wasichana, muendelee kufanya kwa malengo; na nyinyi wazazi mnalazimishwa kuwapatia watoto elimu ya kutosha. Jambo jingine ndio kuendela kuhifadhi haki za wanawake na wasichana kwa ujumla ili kujenga familia yenye matumaini ya kesho,” Bi Kagame alisema.

Raia wa kata ya Cyahinda ambapo tukio lilifanyikia, walisifu namna wanawake wa kijijini huhifadhiwa na kupewa nafasi ya kujitambua na kubadilisha maisha. Nyirabazungu Eugenie alisema kwamba familia yake imemchukuwa yatima na kumtibu kama mototo wao.

Sikukuu ya wanawake wa kijijini ilikuwa sambamba na sikukuu ya watoto wasichana na uhamasishaji juu ya elimu ya watoto. Mandhari ya uhamasishaji ilikuwa inasema, “Tujenge familia nzuri kwa watoto”.

Théogène U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.