kwamamaza 7

Mke wa rais wa Benin katika ziara nchini Rwanda

0

Claudine Talon, mke wa Patrice Talon ambaye ni rais wa Benin alifika Rwanda jana 7 Novemba 2016 katika ziara ya kikazi ya siku nne. Alipofika kwenye uwanja wa ndege wa Kanombe, alipokewa kwa heshima na mwenzake mke wa rais wa Rwanda Bi Jeannette Kagame.

Katika ziara itakayomalizika tarehe 11 Novemba 2016, Claudine Talon atazuru shughuli mbali mbali za mradi wa ‘Imbuto Foundation’ kuhusu maendeleo ya elimu, uhai na vijana.

[ad id=”72″]

Talon anasubiliwa katika hospitali ya Kacyiri na kuizuru Isange One Stop Center, kituo kinachowasaidia waliokatiliwa. Inategemewa kwamba atazuru miradi ya kupambana na maambukizi ya ukimwi kwa wazazi wanaoambukiza watoto na huduma ya uhamasishaji kwa familia zinazoishi na ukimwi.

Mke wa rais wa Benin, Claudine Talon na mwenzake wa rwanda, Jeannette Kagame
Mke wa rais wa Benin, Claudine Talon na mwenzake wa rwanda, Jeannette Kagame

Mke wa rais Claudine atazuru kituo cha kumbukumbu cha waathirika wa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi yalifanyika mnamo mwaka wa 1994.

Rais Patrice Talon anayejulikana kwa kufanya biashara ya pamba, alizuru Rwanda mnamo mwezi wa Agosti; alisifu maendeleo ya nchi ya Rwanda na kusema kwamba uongozi wa Rwanda utachangia kwa mabadiliko ya viongozi barani Afrika.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.