Home HABARI MPYA Mjumbe wa Burundi kwenye Umoja wa Mataifa atakiwa kutokanusha mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi
HABARI MPYA - KIMATAIFA - October 30, 2017

Mjumbe wa Burundi kwenye Umoja wa Mataifa atakiwa kutokanusha mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi

Barozi wa Burundi kwenye umoja wa mataifa,Albert Shingiro atakiwa na mshauri mkuu wa barozi wa Rwanda,Robert Kayinamura kutokanusha mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 baada ya kusema kuwa Rwanda inajifanya nchi iliyoshuhudia mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi.

Akiwa mbele ya kamati ya Umoja wa mataifa ya kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu nchini Burundi na baada ya mkurugenzi wa kamati hii,Fatsah Ouguergouz kueleza kuwa waliyoyaona nchini Burundi ni maajabu, na baada ya hotuba ya waziri na kiongozi makamu wa mjumbe wa Rwanda kwenye Umoaja wa Mataifa,Bakuramutsa Urujeni kusema kwamba Rwanda ina wasiwasi ya maovu yaliyoko Burundi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Barozi Shingiro alieleza kuwa madai haya yote ni kwa ajili za kisiasa na kuongeza kuwa Burundi haina lolote la kuiga kwa Rwanda kwa kuwa Rwanda ilijulikana kwa kutesa wanawake na watoto wao kila usiku na kuwa Rwanda inajifanya kushuhudia mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Rwanda siyo nchi ya kuiga kwa mambo ya kutetea haki za binadamu,wanajiliza kuwa walishuhudia mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi,lakini waliwaua watu miliyoni sita nchini DR Congo”alisema Shingiro.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya,Robert Kayinamura alipiga marufuku madai ya shingiro kwa kumkumbusha kuwa Rwanda siyo iliyofanya ripoti hii na kuwa historia ya Rwanda husika na mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi inajulikana dunia nzima.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hatukujua kwamba mnakanusha mauaji ya kimbali,kuanzia leo tumelewa”alieleza Kayinamura.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.