kwamamaza 7

Mji wa Kigali utampa 50.000 atakayesema nafasi ya majenzi yasio halali

0

Katika maongezi na wanahabari leo juma tano, Parfait Busabizwa, kiongozi anaye husika na uchumi katika mji wa Kigali, amesema ya kuwa kwa ngambo ya kuzuia majenzi yasiyo halali, yule atakaye toa taarifa atakuwa akipewa 50.000 pesa za Rwanda na itakua siri hatajulikana.

Wanao kaa mjini Kigali ni zaidi ya miliyoni 1,2 na hivi inapambana na majenzi mbovu tena bila kibali ya majenzi.

Hadi sasa hesabu huonyesha nyumba 34.000 ambazo zilijengwa kinyume na sheria tena kwa hali mbaya. Mji wa Kigali umesema ya kuwa katika miezi sita viongozi 30 wameazibiwa kwa kuwaficha wanao jenga katika hali isiyo halali.

Kwa ajili ya kupiganisha hayo, wanao ishi Kigali wanaombwa kutoa taarifa mapema na watakuwa wakipewa matabishi.

Yeyote ambaye atahitaji kutoa taarifa ya ukweli bila chuki ataweza kupigia simu ya bila malipo 3262, na wakikuta ni kweli atakuwa napewa matabishi.

Viongozi wa msingi hushotwa vidole ya kuwa wanapewa rushwa ili watu wajenge nafasi isiyo halali tena bila kibali kama vile husema Parfait Busabizwa.

Nyumba 140 ziponajengwa ili walio jenga nafasi mbovu wahamishwe.

Kiongozi huo amesema ya kuwa wilaya tatu ambazo huunda mji wa Kigali Nyarugenge, Gasabo na Kicukiro hujengwa nyumba 140 za vijiji vijulikanavyo kwa jina la IDP Model Villages ambazo zitaishi jamii ambazo ziliishi mahali pabaya.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.