kwamamaza 7

Miss Rwanda aanzisha mashindano ya kuogelea

0

Iradukunda Elsa miss wa Rwanda wa 2017 ameanzisha mashindano ya kugelea ambayo atafanyika kila mwaka.

Mashindano haya ambayo yalifanyanyika kwenye kituo cha michezo cha Cercle Sportif,  yalijumuisha timu nane zikiwemo mojawapo kutoka wilaya ya mashariki na hata mjini Kigali.

Timu ya Cercle Sportif ambayo anaichezea miss Rwanda, Iradukunda Elsa ndiyo iliyoibuka mshindi wa mashindano haya . Timu ya Cercle Sportif inachezewa pia na ndugu wa Miss Iradukunda.

Miss huyo alisema mashindano haya yaliandaliwa kwa madhumuni ya kuendeleza mchezo huu na hasa kuwahamasisha vijana kushiriki.

Miss Rwanda ameandaa mashindano kama sehemu ya miradi aliyoahidi kutekeleza wakati alipokuwa akiwania taji la miss Rwanda la 2017 mapema mwaka huu.

Katika miradi yake ni pamoja na kuhamasisha utumiaji wa bidhaa zinazotengenezewa nyumbani “made in Rwanda” na kuhusiana na mradi huu aliwaatembelea wafanyakazi wa kibinafsi wa wilaya ya Rutsiro na Rubavu.

Miss huyo alisema kuwa, baada ya mashindano hayo, ataendelea kwa kuweka mbele kushughulikia miradi aliyoahidi kukutekeleza wakati alipokuwa akiwania taji hilo ambayo atatekeleza kwa kuwazuru waendashaji shughuli za kibinafsi  na kuwasaidia kupata wadau na wafadhili wa biashara zao.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.