kwamamaza 7

Mipango ya mgombea Frank yapokewa vizuri na vijana

0

Mgombea kwa tiketi ya chama cha Green Dkt.Frank Habineza akiwa akiendesha kampeni wilaya ya Huye ambako aliahidi kuweka nguvu kwenye sera za kuwabadilishia maisha wananchi nakufanya maisha yao kuwa bora. Wananchi nao walionyesha kufurahia mipango yake.

Raia mmoja  aliyekatisha kisomo na ambaye alisema kile anachohisi kuhusu sera za mgombea Frank amesema kwamba sera zake ni za kupokewa vizuri kwa sababu zinalenga kuwanaufaisha vijana.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“ nimeilewa vizuri mipango ya yule mgombea wa chama cha Green, nimeisikia kama mizuri kwa kuwa ametufikiria sisi kama vijana kwa kutusaidia kujiendeleza kupitia sera za kujitaftutia kazi, bila kulipa kodi kwa kipindi cha miaka miwili,na walio na mtaji mdogo wakaondolewa kodi”.

Ameendelea kusifu sera zingine ikiwemo kuwapa chakula bora watoto wa shule za msingi na kusema ni suluhu kwa watoto wanaotoka kwenye familia zisizojiweza.

Sera nyingine ya kuwapa mifugo midogo watoto, Mutuyimana ameieleza kwamba itasaidia watoto kukua wakiwa na imani ya maisha yao ya kesho.

Kijana huyu alikatisha kisomo chake alipokuwa kwenye shule za sekondari darasa la tatu mwaka wa 2016.

Hapa wilaya ya Huye, Dkt. Frank aliwaelezea wananchi mipango mingi ikiwemo mfano wa ada ya kusaidia maisha kwa wanafunzi wa chuo kwa kuahidi kwamba iko ndogo na kwamba ataiongeza kutoka 25,000 hadi 100,000 za faranga za Rwanda.

Pengine atarejesha biashara ya mavazi yaliyovaliwa yanayojulikana kama (chagua) na mabasi madogo.

Mfomo wa bima ya umma(mituelle de santé) nao utaboreshwa kama anavyoadi na watu kuutumia mara baada ya kulipa bila kungojea hadi familia yote imalize kulipa.

Frank aliahidi pia kwamba atabadilisha mji wa Huye kuwa eneo maalum la chimbuko la elimu kama mahali alipowahi kuishi katika maisha yasiyokuwa mazuri kwake wakati alipokuwa anasoma chuo kikuu.

Amesema kuwa pia atawachukulia sawa watu waliosoma katika kifaransa na waliosoma katika kingereza bila kupendelea lugha yoyote katika mitihani ya kazi na kuzipa nguvu sawa katika kufundishwa ili walimu wasije wakaona tatizo kufundisha katika lugha yoyote ile wanayoitaka.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.