kwamamaza 7

Mgombea wa green aonya Kagame wa RPF angefanya kosa atapoteza- Dkt. Frank

0

Dkt. Frank yatangaza kwamba hawakufurahishwa na mambo aliyoyatangaza mgombea wa RPF, Paul Kagame kwamba matokeo ya uchaguzi yamekwisha julikana na kuongeza kwamba wangalifanya kosa lolote yeye atawashinda kwenye uchaguzi.

Dkt. Frank alipewa muda wa kujibu maswali mbalimbali ya redio sauti ya Amerika iliyotangaza habari hii.

Kuhusu suala la kwamba mahali anapokuwa akiendesha kampeni huwa na wafuasi wachache kulingana na hali ilivyo kwa mgombea wa chama cha RPF ambacho huwa na watu chungu nzima.

“Viongozi wa ngazi za serikali wote huwa ni wenyekiti wa chama cha RPF kwenye Kijiji , Eneo , Tarafa, Wilaya na hata jimbo kwa hivyo huwa wanahamasisha watu kuja kwa wingi kuhudhuria, kwa sababu wanawakuta hata nyumbani kwao na kuwachukua kwa magari”. Asema Dkt. Frank.

Kwa hiyo ameongeza kwamba kushinda nao huwa ni vigumu kwa sababu hakuna kiongozi yeyote ambaye angechukua muda wake kuwatolea wito wananchi kuja kuhudhuria kwa ajili yake.

Alitoa  hisia zake kuhusu maneno yaliyotangazwa na rais kagame hivi majuzi.

“Ikiwa anajua kweli alikwisha shinda uchaguzi, anachokeshwa na nini akiendesha kampeni, ona kitita cha fedha ambacho wanalipa kwa ajili ya kampeni, kwa maoni yangu ningesema ni kwa madhumuni ya kuwapa moyo wafuasi wake kwamba watashinda uchaguzi lakini siyo kumaana uchaguzi umekwisha na matokeo yanajulikana”

 

Aliendelea kuonya kwamba na hata rais Kagame anajua bila shaka kwamba angalifanya kosa lolote angejikuta mambo yakimweendea mrama kwa kuwa na hata kwenye chama chake wana watu wengi wanaowafuata na ambao wangejikuta ghafla wakiegamia upande wake wa chama cha Green.

Kwa kuzungumzia pingamizi kwa ujumla amesema kwamba licha ya kuwepo kwa pingamizi hizo zote wanajua kwamba shughuli za kampeni zitaenda vizuri na wataweza kufikia sehemu zote za nchi. “ingawa tuna uwezo mdogo wa kifedha tutajaribu kuutumia kwa kufanya yaliyo muhimu na tuna imani tutazifikia sehemu zote za nchi”

Hapo ndipo alipofichua kwamba wanatumia hata fedha za mkopo wa benki ambapo hata nyumba yake iliwekwa rehani na kusema walifanya uamuzi mwingi wa kujitolea ili shughuli zao za ziweze kufanyika na atakuwa tayari kuipoteza nyumba yake iwapo atashindwa kulipa deni hilo.

Dkt. Frank anazidi kusisitiza kwamba licha ya uhaba wa wanaohudhuria kampeni zake za kuwania kiti cha urais ,angali na matumaini kwamba watashinda uchaguzi wa hapo mwezi Agosti.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.